Zab 29 - Swahili Union Version Bible

Sauti ya Mungu katika DhorubaZaburi ya Daudi.

1 Zab 96:7-9; 1 Nya 16:28,29 Mpeni BWANA, enyi wana wa Mungu,

Mpeni BWANA utukufu na nguvu;

2Mpeni BWANA utukufu wa jina lake;

Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu.

3Sauti ya BWANA i juu ya maji;

Mungu wa utukufu alipiga radi;

BWANA yu juu ya maji mengi.

4Sauti ya BWANA ina nguvu;

Sauti ya BWANA ina adhama;

5Sauti ya BWANA yaivunja mierezi;

Naam, BWANA aivunja-vunja mierezi ya Lebanoni;

6 Zab 114:4; Kum 3:9 Airusha-rusha kama ndama wa ng’ombe;

Lebanoni na Sirioni kama mwana-nyati.

7Sauti ya BWANA yaipasua miali ya moto;

8 Hes 13:26 Sauti ya BWANA yalitetemesha jangwa;

BWANA alitetemesha jangwa la Kadeshi.

9Sauti ya BWANA yawazalisha ayala,

Na kuifichua misitu;

Na ndani ya hekalu lake

Wanasema wote, Utukufu.

10 Zab 93:4 BWANA aliketi juu ya Gharika;

Naam, BWANA ameketi hali ya mfalme milele.

11 Isa 40:29 BWANA atawapa watu wake nguvu;

BWANA atawabariki watu wake kwa amani.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help