Zab 36 - Swahili Union Version Bible

Uovu wa Watu na Wema wa MunguKwa mwimbishaji. Ya Daudi, mtumishi wa Bwana

1 Rum 3:18; Mwa 20:11; Mit 8:13; Mhu 12:3 Kuasi kwake yule mwovu hunena moyoni mwake,

Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake.

2Kwa maana hujipendekeza machoni pake

Kuwa upotovu wake hautaonekana na kuchukiwa.

3 Yer 4:22 Maneno ya kinywa chake ni uovu na hila,

Ameacha kuwa na akili na kutenda mema.

4 Mik 2:1; Isa 65:2 Huwaza maovu kitandani pake,

Hujiweka katika njia mbaya; ubaya hauchukii.

5 Zab 57:10 Ee BWANA, fadhili zako zafika hata mbinguni,

Uaminifu wako hata mawinguni.

6 Ayu 11:8; Rum 11:33; Ayu 7:20; Zab 145:9 Haki yako ni kama milima ya Mungu,

Hukumu zako ni vilindi vikuu,

Ee BWANA, unawaokoa wanadamu na wanyama.

7 Rut 2:12 Ee Mungu, jinsi zilivyo na thamani fadhili zako!

Wanadamu huukimbilia uvuli wa mbawa zako.

8 Ayu 20:17; Ufu 22:1 Watashibishwa kwa unono wa nyumba yako,

Nawe utawanywesha mto wa furaha zako.

9 Isa 12:3; Yer 2:13; Zek 13:1; Yn 4:10,14; Ufu 21:6; Mdo 26:18; Efe 5:8; Kol 1:13; 1 Pet 2:9 Maana kwako Wewe iko chemchemi ya uzima,

Katika nuru yako tutaona nuru.

10 Yer 22:16 Uwadumishie wakujuao fadhili zako,

Na wanyofu wa moyo uaminifu wako.

11Mguu wa kiburi usinikaribie,

Wala mkono wa wasio haki usinifukuze.

12Huko ndiko walikoanguka wafanyao maovu;

Wameangushwa chini wasiweze kusimama.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help