1Nimekuinulia macho yangu,
Wewe uketiye mbinguni.
2Kama vile macho ya watumishi
Kwa mkono wa bwana zao
Kama macho ya mjakazi
Kwa mkono wa bibi yake;
Hivyo macho yetu humwelekea BWANA, Mungu wetu,
Hata atakapoturehemu.
3Uturehemu, Ee BWANA, uturehemu sisi,
Kwa maana tumeshiba dharau.
4Nafsi zetu zimeshiba mzaha wa wenye raha,
Na dharau ya wenye kiburi.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.