1 1 Sam 2:21; Mwa 17:19; 18:10; Gal 4:23 BWANA akamjia Sara kama alivyonena, na BWANA akamfanyia kama alivyosema.
2Ebr 11:11; Mdo 7:8Sara akapata mimba akamzalia Ibrahimu mwana wa kiume katika uzee wake, kwa muhula alioambiwa na Mungu.
3Mwa 17:19Ibrahimu akamwita jina lake Isaka, yule mwana aliyezaliwa, ambaye Sara alimzalia.
4Mwa 17:12; Mdo 7:8Ibrahimu akamtahiri Isaka mwanawe, alipokuwa mwenye siku nane, kama Mungu alivyomwamuru.
5Naye Ibrahimu alikuwa mtu wa miaka mia, alipozaliwa mwana wake Isaka.
6Zab 126:2; Isa 54:1; Lk 1:14,58Sara akasema, Mungu amenifanyia kicheko; kila asikiaye atacheka pamoja nami.
7Mwa 18:11Akasema, N’nani angemwambia Ibrahimu, Sara atanyonyesha wana? Maana nimemzalia mwana katika uzee wake.
Hajiri na Ishmaeli Wafukuzwa8Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya; Ibrahimu akafanya karamu kuu siku ile Isaka alipoachishwa kunyonya.
9Mwa 16:1,4,15; Gal 4:29Sara akamwona yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alimzalia Ibrahimu, anafanya dhihaka.
10Gal 4:29-30; Mwa 25:6; 36:6,7Kwa hiyo akamwambia Ibrahimu, Mfukuze mjakazi huyu na mwanawe, maana mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka.
11Mwa 17:18Na neno hilo lilikuwa baya sana machoni pa Ibrahimu, kwa ajili ya mwanawe.
12Rum 9:7; Ebr 11:18Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa.
13Mwa 16:10; 17:20; 25:12Naye mwana wa mjakazi nitamfanya kuwa taifa, maana huyu naye ni uzao wako.
14 Yn 8:35 Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akimtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba.
15Hes 20:5; Zab 63:1Yale maji yakaisha katika kiriba, akamlaza kijana chini ya kijiti kimoja.
16Mwa 44:34Akaenda akakaa akimkabili, mbali naye kadiri ya mtupo wa mshale; maana alisema, Nisimwone kijana akifa; naye akakaa akimkabili, akapaza sauti yake, akalia.
17Kut 3:7; 2 Fal 13:4,23Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko.
18Mwa 21:13; 25:12; Amu 8:24Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa.
19Hes 22:31; 2 Fal 6:17; Lk 24:16Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana.
20 Mwa 16:12; 39:2,3 Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde.
21Mwa 24:4; 20:2; 26:28; Isa 8:10Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke katika nchi ya Misri.
Abrahamu na Abimeleki Wawekeana Agano22 Mwa 26:26 Ikawa wakati ule Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakamwambia Ibrahimu, wakinena, Mungu yu pamoja nawe katika yote unayotenda.
23Yos 2:12; 1 Sam 24:21Basi sasa uniapie kwa Mungu, ya kuwa hutanitenda hila, wala mwanangu, wala mjukuu wangu, lakini kwa kadiri ya fadhili niliyokutendea utanitendea mimi, na nchi hii ambayo umetembea ndani yake.
24Ibrahimu akasema, Nitaapa.
25 Mwa 26:15-22 Kisha Ibrahimu akamlaumu Abimeleki kwa sababu ya kisima cha maji ambacho watumwa wa Abimeleki wamekinyang’anya.
26Abimeleki akasema, Mimi sijui ni nani aliyetenda neno hili, wala hukuniambia, wala sikusikia habari hii ila leo tu.
27Mwa 26:28-31Ibrahimu akatwaa kondoo na ng’ombe akampa Abimeleki, na hao wawili wakafanya mapatano.
28Ibrahimu akaweka wana kondoo wa kike saba peke yao.
29Mwa 33:8Abimeleki akamwambia Ibrahimu, Hawa wana kondoo wa kike saba, uliowaweka peke yao, maana yake nini?
30Mwa 31:48Akasema, Hawa wana kondoo wa kike saba utawapokea mkononi mwangu, wawe ushuhuda ya kuwa ni mimi niliyekichimba kisima hiki.
31Mwa 26:33Kwa hiyo akapaita mahali pale Beer-sheba, kwa sababu waliapa huko wote wawili.
32Yos 13:2Basi wakafanya mapatano huko Beer-sheba. Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakaondoka wakarudi hata nchi ya Wafilisti.
33Kum 33:27; Zab 9:7; Isa 9:6; Rum 16:26; Ebr 13:8; 1 Tim 1:17; Ufu 10:6Ibrahimu akapanda mkwaju huko Beer-sheba, akaliitia huko jina la BWANA Mungu wa milele.
34Ibrahimu akakaa hali ya ugeni katika nchi ya Wafilisti siku nyingi.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.