1 Isa 26:20 Unirehemu, Ee Mungu, unirehemu mimi,
Maana nafsi yangu imekukimbilia Wewe.
Nitaukimbilia uvuli wa mbawa zako,
Hata misiba hii itakapopita.
2 Zab 138:8 Nitamwita MUNGU Aliye juu,
Mungu anitimiziaye mambo yangu.
3 Zab 144:5; 40:11 Atapeleka toka mbinguni na kuniokoa,
Atukanapo yule atakaye kunimeza.
Mungu atazipeleka
Fadhili zake na kweli yake
4 Mit 30:14; Zab 64:3 Nafsi yangu i kati ya simba,
Nitastarehe kati yao waliowaka moto.
Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale,
Na ndimi zao ni upanga mkali.
5 Zab 108:5 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,
Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.
6 Zab 9:15 Wameweka wavu ili kuninasa miguu;
Nafsi yangu imeinama;
Wamechimba shimo mbele yangu;
Wametumbukia ndani yake!
7 Zab 108:1 Ee Mungu, moyo wangu u thabiti,
Moyo wangu u thabiti.
Nitaimba, nitaimba zaburi,
8 Amu 5:12 Amka, utukufu wangu.
Amka, kinanda na kinubi,
Nitaamka alfajiri.
9Ee Bwana, nitakushukuru kati ya watu,
Nitakuimbia zaburi kati ya mataifa.
10 Zab 108:4 Maana fadhili zako ni kubwa hata mbinguni,
Na uaminifu wako hata mawinguni.
11Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,
Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.