1Msingi wake upo
Juu ya milima mitakatifu.
2BWANA ayapenda malango ya Sayuni
Kuliko maskani zote za Yakobo.
3 Isa 60:1 Umetajwa kwa mambo matukufu,
Ee Mji wa Mungu.
4Nitataja Rahabu na Babeli
Miongoni mwao wanaonijua.
Tazama Filisti, na Tiro, na Kushi;
Huyu alizaliwa humo.
5 Eze 48:35; Mt 16:18 Naam, mintarafu Sayuni itasemwa,
Huyu na huyu alizaliwa humo.
Na Yeye Aliye juu
Ataufanya imara.
6 Zab 22:30; Isa 4:3; Yer 3:19; Eze 13:9 BWANA atahesabu, awaandikapo mataifa,
Huyu alizaliwa humo.
7Waimbao na wachezao na waseme,
Visima vyangu vyote vimo mwako.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.