Amu UTANGULIZI - Swahili Union Version Bible

UTANGULIZIBaada ya Yoshua hakutokea mtu wa kurithi nafasi ya kuliongoza taifa la Israeli. Viongozi waliojitokeza walikuwa mashujaa walioongoza majeshi ya makabila yao katika vita vilivyokumba sehemu zao. Wakati wa amani viongozi hao walitawala sehemu zilizohusika na kila kabila lilishughlikia mambo yake. Viongozi hao wa kijeshi wanaitwa Waamuzi ambao huenda waliongoza makabila ya Waisraeli kwa kipindi cha miaka kama mia tatu na hamsini.Kitabu hiki kinaitwa cha Waamuzi kwa kuwa masimulizi yake yanahusu viongozi wa kijeshi kumi na nane walioitwa jina hilo.Katika Kitabu cha Waamuzi tunasimuliwa kuwa Waisraeli walipoingia katika nchi ya Ahadi hawakuiteka nchi hiyo yote mara moja. Sehemu fulani walishindwa kupaingia na nyingine walilazimika kukaa na makabila yaliyokuwa maadui wao. Aidha Waisraeli mara kwa mara walimuasi Mungu wakaiga desturi za dini za Wakanaani na kwa sababu ya uasi huo Mungu aliwaacha. Maadui walipohisi udhaifu wa kabila fulani la Waisraeli walilishambulia (3:1-8). Waisraeli walipotubu na kumlilia BWANA, Mungu aliwahurumia akamtuma kiongozi wa kijeshi aitwaye mwamuzi, wakashinda maadui akawaokoa (2:11-16; 3:9-15; 4:1-4; 6:1-10; 10:6-16; 31:1). Mungu aishiye milele ni wa upendo na huruma. Mwenye dhambi akitubu husamehewa. Ushindi wa Waisraeli haukutokana na uwezo wao bali uwezo wa Mungu. Kumtegemea Mungu, kutii Agano na maisha ya dini yao kuwa kitovu cha taifa ni mambo yaliyokosekana wakati huo hadi utawala wa kifalme ulipoanzishwa.Yaliyomo:1. Maelezo kuhusu ushindi wa Yoshua, Sura 1:1–2:102. Waamuzi wa Waisraeli, Sura 2:11–16:313. Machafuko katika Israeli, Sura 17–21
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help