Zab 65 - Swahili Union Version Bible

Shukrani kwa Mavuno MengiKwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Wimbo.

1Ee Mungu, sifa zakulaiki katika Sayuni,

Na kwako Wewe itaondolewa nadhiri.

2 Lk 11:9,10; Isa 66:23 Wewe usikiaye kuomba,

Wote wenye mwili watakujia.

3 Ebr 9:14 Ingawa maovu mengi yanamshinda,

Wewe utayafunika maasi yetu.

4 Zab 33:12 Heri mtu yule umchaguaye,

Na kumkaribisha akae nyuani mwako.

Na tushibe wema wa nyumba yako,

Patakatifu pa hekalu lako.

5Kwa mambo ya kutisha utatujibu,

Katika haki, Ee Mungu wa wokovu wetu.

Wewe uliye tumaini la miisho yote ya dunia,

Na la bahari iliyo mbali sana,

6Milima waiweka imara kwa nguvu zako,

Huku ukijifunga uweza kama mshipi.

7 Mt 8:26 Wautuliza uvumi wa bahari,

Uvumi wa mawimbi yake,

Na ghasia ya mataifa;

8 Ayu 37:5 Kwa hiyo wakaao mbali kabisa huogopa ishara zako;

Milango ya asubuhi na jioni waifurahisha.

9Umeijilia nchi na kuisitawisha,

Umeitajirisha sana;

Mto wa Mungu umejaa maji;

Wawaruzuku watu nafaka

Maana ndiwe uitengenezaye ardhi.

10Matuta yake wayajaza maji;

Wapasawazisha palipoinuka,

Wailainisha nchi kwa manyunyu;

Waibariki mimea yake.

11 Zab 104:3 Umeuvika mwaka taji ya wema wako;

Mapito yako yadondoza unono.

12Huyadondokea malisho ya nyikani,

Na vilima vyajifunga furaha.

13Na malisho yamevikwa kondoo,

Na mabonde yamepambwa nafaka,

Yanashangilia, naam, yanaimba.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help