1Nafsi yangu yamngoja Mungu peke yake kwa kimya,
Wokovu wangu hutoka kwake.
2Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu,
Ngome yangu, sitatikisika sana.
3 Isa 30:13 Hata lini mtamshambulia mtu,
Mpate kumwua ninyi nyote pamoja?
Kama ukuta unaoinama,
Kama kitalu kilicho tayari kuanguka,
4 Zab 28:3 Hufanya shauri kumwangusha tu katika cheo chake;
Huufurahia uongo.
Kwa kinywa chao hubariki;
Kwa moyo wao hulaani.
5 Mik 7:7,10 Nafsi yangu, umngoje Mungu peke yake kwa kimya.
Tumaini langu hutoka kwake.
6Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu,
Ngome yangu, sitatikisika sana.
7 Yer 3:23 Kwa Mungu wokovu wangu,
Na utukufu wangu;
Mwamba wa nguvu zangu,
Na kimbilio langu ni kwa Mungu.
8 1 Sam 1:15; Zab 42:4 Enyi watu, mtumainini sikuzote,
Ifunueni mioyo yenu mbele zake;
Mungu ndiye kimbilio letu.
9Hakika binadamu ni ubatili,
Na wenye cheo ni uongo,
Katika mizani huinuka;
Wote pamoja ni hafifu kuliko ubatili.
10 Isa 26:4; Mk 10:23; Lk 12:15 Msiitumainie dhuluma,
Wala msijivune kwa unyang’anyi;
Mali izidipo msiiangalie sana moyoni.
11Mara moja amenena Mungu;
Mara mbili nimeyasikia haya,
Ya kuwa nguvu zina Mungu,
12 Ayu 34:11; Yer 17:10; Mt 16:27; 1 Pet 1:17; Rum 2:6; Ufu 2:23 Na fadhili ziko kwako, Ee Bwana;
Maana ndiwe umlipaye kila mtu
Sawasawa na haki yake.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.