Zab 97 - Swahili Union Version Bible

Utukufu wa Enzi ya Mungu

1BWANA ametamalaki, nchi na ishangilie,

Visiwa vingi na vifurahi.

2Mawingu na giza vyamzunguka,

Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake.

3 Dan 7:10; Hab 3:5 Moto hutangulia mbele zake,

Nao huwateketeza watesi wake pande zote.

4Umeme wake uliuangaza ulimwengu,

Nchi ikaona ikatetemeka.

5Milima iliyeyuka kama nta mbele za BWANA,

Mbele za Bwana wa dunia yote.

6Mbingu zimetangaza haki yake,

Na watu wote wameuona utukufu wake.

7 Kut 20:4; Law 26:1; Isa 37:18,19; Yer 10:14; Ebr 1:6 Na waaibishwe wote waabuduo sanamu,

Wajivunao kwa vitu visivyofaa;

Enyi miungu yote, msujuduni Yeye.

8Sayuni imesikia na kufurahi,

Binti za Yuda walishangilia,

Kwa sababu ya hukumu zako, Ee BWANA.

9 Efe 1:21 Maana Wewe, BWANA, ndiwe Uliye juu,

Juu sana kuliko nchi yote;

Umetukuka sana juu ya miungu yote.

10 Zab 101:3; Amo 5:15; Rum 7:15; 1 Sam 2:9; Mit 2:8; Dan 3:28 Enyi mmpendao BWANA, uchukieni uovu;

Huwalinda nafsi zao watauwa wake,

Na kuwaokoa na mkono wa wasio haki.

11Nuru imemzukia mwenye haki,

Na furaha wanyofu wa moyo.

12Enyi wenye haki, mmfurahieni BWANA,

Na kulishukuru jina lake takatifu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help