Sef 2 - Swahili Union Version Bible

Hukumu kwa Adui wa Israeli

1 Yoe 2:16 Jikusanyeni, naam, jikusanyeni, Ee taifa lisilo na haya;

22 Fal 23:26kabla haijazaa hiyo amri, kabla haijapita siku ile kama makapi, kabla haijawajilia hasira kali ya BWANA, kabla haijawajilia siku ya hasira ya BWANA.

3Amo 5:6,15; Zab 76:9; Yoe 2:14Mtafuteni BWANA, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitenda hukumu zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya BWANA.

4 Yer 6:4; Isa 14:29-31; Yer 47:1-7; Eze 25:15-17; Yoe 3:4-8 Kwa kuwa Gaza utaachwa, na Ashkeloni utakuwa ukiwa; wataufukuzia mbali Ashdodi wakati wa adhuhuri, na Ekroni utang’olewa. Amo 1:6-8; Zek 9:5-7

5Eze 25:16; Yos 13:3Ole wao wakaao karibu na pwani ya bahari, taifa la Wakerethi! Neno la BWANA li juu yenu, Ee Kanaani, nchi ya Wafilisti; mimi nitakuangamiza, asibaki mtu akaaye kwako.

6Isa 17:2Na hiyo nchi ya pwani itakuwa malisho, yenye vibanda vya wachungaji, na mazizi ya makundi ya kondoo.

7Isa 11:11; Hag 1:12; Mik 5:7; 4:10; Kut 4:31; Lk 1:68; Zab 126:4; Yer 23:3; Eze 39:25Na hiyo nchi ya pwani itakuwa nchi ya watu wa nyumba ya Yuda waliosalia; watalisha makundi yao huko; watalala katika nyumba za Ashkeloni wakati wa jioni; kwa maana BWANA, Mungu wao, atawajilia na kuwarudisha wafungwa wao.

8Isa 15:1—16:14; 25:10-12; Yer 48:1—49:6; EzeMimi nimeyasikia matukano ya Moabu, na dhihaka za wana wa Amoni, ambazo kwa hizo wamewatukana watu wangu, na kujitukuza juu ya mpaka wao. 21:28-32; 25:1-11; Amo 1:13-15

9Isa 15:1; Amo 2:1; 1:13; Mwa 19:24Basi kama niishivyo, asema BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, Hakika Moabu atakuwa kama Sodoma, na wana wa Amoni kama Gomora, yaani, milki ya upupu, na mashimo ya chumvi, ukiwa wa daima; watu wangu waliosalia watawateka nyara, na watu wa taifa langu waliobaki watawarithi.

10Mambo hayo yatawapata kwa sababu ya kiburi chao, kwa kuwa wamewatukana watu wa BWANA wa majeshi, na kujitukuza juu yao.

11Mwa 49:10; 10:5; Zab 2:8; 22:27; Isa 2:2,3; 11:9,10; Mal 1:1; Yn 4:21; 1 Tim 2:8BWANA atakuwa mwenye kuwatisha sana; kwa maana atawafisha kwa njaa miungu yote ya dunia; na watu watamsujudia yeye, kila mtu toka mahali pake; naam, nchi zote za mataifa.

12Isa 18:1-7Na ninyi Wakushi pia, mtauawa kwa upanga wangu.

13Isa 10:5-34; 14:24-27; Nah 1:1—3:19Naye atanyosha mkono wake juu ya upande wa kaskazini, na kuiangamiza Ashuru; naye ataufanya Ninawi kuwa ukiwa, kuwa mahali pakavu kama jangwa.

14Isa 13:21Na makundi ya wanyama watalala kati yake, wanyama wote wa mataifa; mwari-nyuni na nungu watakaa juu ya vichwa vya nguzo zake; sauti yao itasikiwa madirishani; vizingitini mwake mtakuwa ukiwa; kwa maana ameifunua kazi ya mierezi.

15 Isa 47:8; Ufu 18:7 Huu ndio mji ule wa furaha,

Uliokaa pasipo kufikiri,

Uliosema moyoni mwake, Mimi niko,

Wala hapana mwingine ila mimi.

Jinsi ulivyokuwa ukiwa,

Mahali pa kulala pa wanyama wa bara!

Kila mtu apitaye atazomea,

Na kutikisa mkono wake.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help