Zab 49 - Swahili Union Version Bible

Upumbavu wa Kutegemea MaliKwa mwimbishaji. Ya Wakorahi. Zaburi.

1Sikieni haya, enyi mataifa yote;

Sikilizeni, ninyi nyote mnaokaa duniani.

2Watu wakuu na watu wadogo wote pia,

Tajiri na maskini wote pamoja.

3Kinywa changu kitanena hekima,

Na fikira za moyo wangu zitakuwa za busara.

4 Zab 78:2 Nitatega sikio langu nisikie mithali,

Na kufumbua fumbo langu kwa kinubi

5Kwa nini niogope siku za uovu,

Ubaya ukinizunguka miguuni pangu?

6Wa hao wanaozitumainia mali zao,

Na kujisifia wingi wa utajiri wao;

7 Mt 16:26 Hakuna mtu awezaye kumkomboa ndugu yake,

Wala kumpa Mungu fidia kwa ajili yake,

8 Ayu 36:18 (Maana fidia ya nafsi zao ina gharama,

Wala hana budi kuiacha hata milele;)

9 Ebr 9:27; Zab 89:48 ili aishi sikuzote asilione kaburi.

10Naam, ataliona, hata wenye hekima hufa;

Mpumbavu na mjinga hupotea pamoja,

Na kuwaachia wengine mali zao.

11Makaburi ni nyumba zao hata milele,

Maskani zao vizazi hata vizazi.

Hao waliotaja mashamba yao

Kwa majina yao wenyewe.

12Lakini mwanadamu hadumu katika heshima,

Bali amefanana na wanyama wapoteao.

13Hiyo ndiyo njia yao, ujinga wao,

Nao walioko baada yao huyaridhia maneno yao.

14 Dan 7:22; Mal 4:3; Lk 22:30; 1 Kor 6:2; 2 Tim 2:12; Ufu 2:26 Kama kondoo wamewekwa kwenda kuzimu,

Na mauti itawachunga;

Watu wanyofu watawamiliki asubuhi;

Umbo lao litachakaa, kao lao ni kuzimu.

15 Hos 13:14 Bali Mungu atanikomboa nafsi yangu,

Atanitoa mkononi mwa kuzimu, maana atanikaribisha.

16Usiogope mtu atakapopata utajiri,

Na fahari ya nyumba yake itakapozidi.

17Maana atakapokufa hatachukua cho chote;

Utukufu wake hautashuka ukimfuata.

18Ajapojibariki nafsi yake alipokuwa hai,

Na watu watakusifu ukijitendea mema,

19Atakwenda kwenye kizazi cha baba zake

Hawataona nuru hata milele.

20 Mhu 3:19-21 Mwanadamu mwenye heshima, iwapo hana akili,

Amefanana na wanyama wapoteao.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help