1Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo.
2 na nchi yako Beula; kwa kuwa BWANA anakufurahia, na nchi yako itaolewa.
5Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe.
6 Wim 3:3; Isa 52:8; Eze 3:17; Ebr 13:17 Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha BWANA, msiwe na kimya;
7Isa 61:11; Sef 3:20wala msimwache akae kimya, mpaka atakapoufanya imara Yerusalemu, na kuufanya kuwa sifa duniani.
8Kum 28:31; Yer 5:17BWANA ameapa kwa mkono wake wa kuume, na kwa mkono wa nguvu zake, Hakika sitawapa adui zako nafaka yako tena kuwa chakula chao; wala wageni hawatakunywa divai yako, uliyoifanyia kazi.
9Kum 12:12Lakini walioivuna, ndio watakaoila, na kumhimidi BWANA; na walioichuma, ndio watakaoinywa, ndani ya nyua za patakatifu pangu.
10Piteni, piteni, katika malango;
Itengenezeni njia ya watu;
Tutieni, tutieni barabara; toeni mawe yake;
Twekeni bendera kwa ajili ya kabila za watu.
11 Zek 9:9; Mt 21:5; Yn 12:15; Isa 40:10; 49:4; Ufu 22:12 Tazama, BWANA ametangaza habari mpaka mwisho wa dunia,
Mwambieni binti Sayuni,
Tazama, wokovu wako unakuja;
Tazama, thawabu yake i pamoja naye,
Na malipo yake yako mbele zake.
12Nao watawaita, Watu watakatifu,
Waliokombolewa na BWANA;
Nawe utaitwa, Aliyetafutwa,
Mji usioachwa.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.