1 Pet 2 - Swahili Union Version Bible

Jiwe Hai na Watu Walioteuliwa

1 Efe 4:22; Yak 1:21 Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote.

21 Kor 3:2; Ebr 5:12,13; Mt 18:3Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;

3Zab 34:8ikiwa mmeonja ya kwamba Bwana ni mwenye fadhili.

4Zab 118:22; Isa 28:16; Mt 21:42; Mdo 4:11Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima.

5Efe 2:21,22; Rum 12:1Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.

6Isa 28:16; Rum 9:33Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko

Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima,

Na kila amwaminiye hatatahayarika.

7 Zab 118:22; Mt 21:42 Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini,

Jiwe walilolikataa waashi,

Limekuwa jiwe kuu la pembeni.

8 Isa 8:14-15; Rum 9:33 Tena,

Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha.

Kwa maana hujikwaza kwa neno lile, wasiliamini, nao waliwekwa kusudi wapate hayo.

9Kut 19:5-6; Isa 43:20-21; Kum 4:20; 7:6; 14:2; Tit 2:14; Isa 9:2; Mdo 26:18; 2 Kor 4:6; Efe 5:8; Flp 2:15; Ufu 1:6Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;

10Hos 1:6,9; 2:1,23; Rum 9:25ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.

Ishini kama Watumishi wa Mungu

11 Zab 39:12; Gal 5:17,24; Efe 2:19; Yak 4:1 Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.

12Isa 10:3; Mt 5:16; Yak 3:13Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.

13 Rum 13:1-7; Tit 3:1 Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana; ikiwa ni mfalme, kama mwenye cheo kikubwa;

14ikiwa ni wakubwa, kama wanaotumwa naye ili kuwalipiza kisasi watenda mabaya na kuwasifu watenda mema.

151 Pet 3:16Kwa sababu ndiyo mapenzi ya Mungu, kwamba kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu;

16Gal 5:13kama walio huru, ila wasioutumia uhuru huo kwa kusitiri ubaya, bali kama watumwa wa Mungu.

17Rum 12:10; Mit 24:21; Mt 22:21Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme.

Mfano wa Kuteswa kwa Yesu

18 Efe 6:5; Tit 2:9 Enyi watumishi, watiini bwana zenu kwa hofu nyingi, sio wao walio wema na wenye upole tu, bali nao walio wakali.

19Maana huu ndio wema hasa, mtu akivumilia huzuni kwa kumkumbuka Mungu, pale ateswapo isivyo haki.

201 Pet 3:14,17; 4:13,14; Mt 5:10Kwa maana ni sifa gani kustahimili, mtendapo dhambi na kupigwa makofi? Lakini kustahimili, mtendapo mema na kupata mateso, huu ndio wema hasa mbele za Mungu.

21Mt 16:24; Yn 13:15Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.

22Isa 53:9; Yn 8:46; 2 Kor 5:21Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake.

23Isa 53:7Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.

24Isa 53:5,12; 1 Yoh 3:5; Rum 6:11; Ebr 9:28Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.

25Isa 53:6; Eze 34:5; 1 Pet 5:4; Yn 10:12Kwa maana mlikuwa mnapotea kama kondoo; lakini sasa mmemrudia Mchungaji na Mwangalizi wa roho zenu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help