Kut 16 - Swahili Union Version Bible

Mkate kutoka Mbinguni

1 kama hesabu ya watu wenu ilivyo; ndivyo mtakavyotwaa, kila mtu kwa ajili ya hao walioko hemani mwake.

17Wana wa Israeli wakafanya hivyo, wakaokota wengine zaidi, wengine kupungua.

182 Kor 8:15Nao walipoipima kwa pishi, yeye aliyekuwa ameokota kingi hakubakiwa na kitu, na yeye aliyekuwa ameokota kichache hakupungukiwa; wakaokota kila mtu kama ulaji wake ulivyokuwa.

19Musa akawaambia, Mtu awaye yote asikisaze hata asubuhi.

20Lakini hawakumsikiza Musa; wengine miongoni mwao wakakisaza hata asubuhi, nacho kikaingia mabuu na kutoa uvundo; Musa akawakasirikia sana.

21Basi wakaokota asubuhi baada ya asubuhi, kila mtu kama ulaji wake ulivyokuwa; na hapo jua lilipokuwa ni kali, kikayeyuka.

22Basi ikawa siku ya sita wakaokota kile chakula sehemu maradufu, kila mtu pishi mbili; na wazee wote wa mkutano wakaenda na kumwambia Musa.

23Kut 20:8; 31:15; 35:3; Mwa 2:3; Law 23:3Akawaambia, Ndilo neno alilonena BWANA Kesho ni starehe takatifu, Sabato takatifu kwa BWANA; okeni mtakachooka, na kutokosa mtakachotokosa; na hicho kitakachowasalia jiwekeeni kilindwe hata asubuhi.

24Kut 16:20Basi wakakiweka hata asubuhi, kama Musa alivyowaagiza; nacho hakikutoa uvundo wala kuingia mabuu.

25Ebr 4:4; Mt 12:12; 24:20Musa akasema, Haya, kuleni hiki leo; kwa kuwa leo ni Sabato ya BWANA; leo hamtakiona nje barani.

26Kut 20:9,10Siku sita mtaokota; lakini siku ya saba ni Sabato, siku hiyo hakitapatikana.

27Ikawa siku ya saba wengine wakatoka kwenda kukiokota, wasikione.

282 Fal 17:14; Zab 78:10,22; 106:13; Yer 4:14BWANA akamwambia Musa, Mtakataa kuyashika maagizo yangu na sheria zangu hata lini?

29Angalieni, kwa kuwa BWANA amewapa ninyi hiyo Sabato, kwa sababu hii huwapa siku ya sita chakula cha siku mbili; kaeni kila mtu mahali pake, mtu awaye yote asiondoke mahali pake kwa siku ya saba.

30Basi hao watu wakapumzika kwa siku ya saba.

31Hes 11:7-8Na nyumba ya Israeli wakakiita jina lake Mana; nacho kilikuwa mfano wa chembe za mtama, nyeupe; na tamu yake ilikuwa kama tamu ya maandazi membamba yaliyoandaliwa kwa asali.

32Musa akasema, Hili ni neno BWANA aliloliamuru, Pishi moja ya kitu hicho na kiwekwe kwa ajili ya vizazi vyenu; ili kwamba wao wapate kukiona kile chakula nilichowalisha ninyi barani, hapo nilipowaleta kutoka nchi ya Misri.

33Ebr 9:4Basi Musa akamwambia Haruni, Twaa kopo, ukatie pishi moja ya hiyo Mana ndani yake, uiweke mbele ya BWANA, ilindwe kwa ajili ya vizazi vyenu.

34Kut 25:16,21; 40:20; Hes 17:10; Kum 10:5; 1 Fal 8:9Kama vile BWANA alivyomwagizia Musa ndivyo Haruni alivyoiweka hapo mbele ya Ushahidi, ili ilindwe.

35Yos 5:12; Hes 33:38; Kum 8:2,3; Neh 9:20,21; Yn 6:31,49Na wana wa Israeli walikula Mana muda wa miaka arobaini, hata walipofikilia nchi iliyo na watu, wakala ile Mana, hata walipofikilia mipakani mwa nchi ya Kanaani.

36Hiyo omeri ni sehemu kumi ya efa.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help