Zab 64 - Swahili Union Version Bible

Sala ya Ulinzi kutoka kwa AduiKwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

1Mungu, uisikie sauti yangu katika malalamiko yangu;

Unilinde uhai wangu na hofu ya adui.

2 Zab 143:9 Utanificha mbali na shauri la siri la watenda mabaya,

Mbali na ghasia ya watu wafanyao maovu;

3 Zab 57:4 Waliounoa ulimi wao kama upanga,

Wameielekeza mishale yao, maneno ya uchungu,

4Wapate kumpiga mkamilifu faraghani,

Kwa ghafula humpiga wala hawaogopi.

5Walijifanya hodari katika jambo baya;

Hushauriana juu ya kutega mitego;

Husema, Ni nani atakayeiona?

6Hutunga maovu; husema, Tumefanya shauri kamili;

Na mawazo ya ndani ya kila mmoja wao,

Na moyo wake, huwa siri kabisa.

7Kwa hiyo Mungu atawapiga shabaha,

Kwa mshale mara watapigwa.

8 Mit 12:13 Ndivyo watakavyokwazwa,

Ulimi wao wenyewe ukishindana nao.

Wote wawaonao watatikisa kichwa.

9Na watu wote wataogopa,

Wataitangaza kazi ya Mungu,

Na kuyafahamu matendo yake.

10 Zab 32:11; Flp 4:4 Mwenye haki atamfurahia BWANA na kumkimbilia,

Na wote wenye moyo wa adili watajisifu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help