Yos 3 - Swahili Union Version Bible

Waisraeli Wavuka Yordani

1 Hes 25:1; 33:49; Yos 2:1 Yoshua akaondoka asubuhi na mapema, nao wakatoka Shitimu, wakafika mto wa Yordani, yeye na wana wa Israeli wote, wakakaa hapo kabla ya kuvuka.

2Yos 1:10,11Ikawa baada ya siku tatu, maakida wakapita katikati ya marago,

3Hes 10:33; Kum 31:9wakawaamuru watu wote wakisema, Mtakapoliona sanduku la agano la BWANA, Mungu wenu, na makuhani Walawi wakilichukua, ndipo mtakapoondoka hapa mlipo na kulifuata.

4Kut 19:12; Kum 28:58; 1 Nya 16:30; Zab 2:11; 96:9; Ebr 12:28Lakini, na iwe nafasi kati ya ninyi na lile sanduku, kama dhiraa elfu mbili kiasi chake; msilikaribie mpate kuijua njia ambayo hamna budi kuiendea; kwa maana hamjapita njia hii bado.

5Kut 10:10; Law 20:7; Hes 11:18; Yos 7:13; 1 Sam 16:5; Yoe 2:16Yoshua akawaambia watu, Jitakaseni; maana kesho BWANA atatenda mambo ya ajabu kati yenu.

6Hes 4:15Kisha Yoshua akawaambia makuhani, akasema, Liinueni sanduku la agano, mkavuke mbele ya hao watu. Wakaliinua sanduku la agano, wakatangulia mbele ya watu.

7Yos 4:14; 1 Nya 29:25; 2 Nya 1:1BWANA akamwambia Yoshua, Hivi leo nitaanza kukutukuza mbele ya Israeli wote, wapate kujua ya kuwa mimi nitakuwa pamoja na wewe, kama nilivyokuwa pamoja na Musa.

8Nawe uwaamuru hao makuhani walichukuao sanduku la agano, ukawaambie, Mtakapofika ukingo wa maji ya Yordani, simameni katika Yordani.

9Basi Yoshua akawaambia wana wa Israeli, Njoni huku, mkayasikie maneno ya BWANA, Mungu wenu.

10Kum 5:26; 1 Sam 17:26; 2 Fal 19:4; Hos 1:10; Mt 16:16; 1 The 1:9; Kut 33:2; Kum 7:1; Zab 44:2Yoshua akasema, Kwa jambo hili mtajua ya kuwa Mungu aliye hai yu kati yenu, na ya kuwa hatakosa kuwatoa mbele yenu Mkanaani, na Mhiti, na Mhivi, na Mperizi, na Mgirgashi, na Mwamori, na Myebusi.

11Zab 24:1; Ayu 41:11; Mik 4:13; Zek 4:14; 6:5Tazama, sanduku la agano la Bwana wa dunia yote linavuka mbele yenu na kuingia Yordani.

12Yos 4:2Basi sasa twaeni watu kumi na wawili katika kabila za Israeli, kila kabila mtu mmoja.

13Kut 15:8; Zab 78:13; 114:3; Hab 3:15Itakuwa, wakati nyayo za makuhani walichukuao sanduku la BWANA, Bwana wa dunia yote, zitakaposimama katika maji ya Yordani, hayo maji ya Yordani yatatindika, maji yale yashukayo kutoka juu; nayo yatasimama kama chuguu.

14Kut 25:10; 26:30; Hes 10:3; 2 Nya 6:41; Zab 132:8; Mdo 7:45; Ebr 9:4Hata ikawa, hao watu walipotoka katika hema zao, ili kuvuka Yordani, makuhani waliolichukua sanduku la agano wakatangulia mbele ya watu,

151 Nya 12:15; Yer 12:5; 49:19; Yos 4:18; 5:10,12basi hao waliolichukua hilo sanduku walipofika Yordani, na nyayo za makuhani waliolichukua sanduku zilipotiwa katika maji ya ukingoni, (maana Yordani hujaa hata kingo zake na kufurika wakati wote wa mavuno),

161 Fal 4:12; 7:46; Kum 3:17; Mwa 14:3; Hes 34:3ndipo hayo maji yaliyoshuka kutoka juu yakasimama, yakainuka, yakawa chuguu, mbali sana, huko Adamu, mji ule ulio karibu na Sarethani, na maji yale yaliyotelemkia bahari ya Araba, yaani Bahari ya Chumvi, yakatindika kabisa; watu wakavuka kukabili Yeriko.

17Kut 14:29; Ebr 11:29Na hao makuhani waliolichukua sanduku la agano la BWANA wakasimama imara mahali pakavu katikati ya Yordani; Israeli wote wakavuka katika nchi kavu, hata taifa lile lote likaisha kuvuka Yordani.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help