Zab 30 - Swahili Union Version Bible

Shukrani kwa Kuponywa Maradhi MabayaZaburi. Wimbo wa kuweka wakfu hekalu. Ya Daudi.

1Ee BWANA, nitakutukuza kwa maana umeniinua,

Wala hukuwafurahisha adui zangu juu yangu.

2 Zab 6:2-4 Ee BWANA, Mungu wangu,

Nalikulilia ukaniponya.

3 Zab 40:1,2 Umeniinua nafsi yangu,

Ee BWANA, kutoka kuzimu.

Umenihuisha na kunitoa

Miongoni mwao washukao shimoni.

4Mwimbieni BWANA zaburi,

Enyi watauwa wake.

Na kufanya shukrani.

Kwa kumbukumbu la utakatifu wake.

5 Zab 16:11; Ufu 22:17 Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo,

Katika radhi yake mna uhai.

Huenda kilio huja kukaa usiku,

Lakini asubuhi huwa furaha.

6 Ayu 29:18 Nami nilipofanikiwa nalisema,

Sitaondoshwa milele.

7 Zab 104:29 BWANA, kwa radhi yako

Wewe uliuimarisha mlima wangu.

Uliuficha uso wako,

Nami nikafadhaika.

8Ee BWANA, nalikulilia Wewe,

Naam, kwa BWANA naliomba dua.

9 Zab 115:17 Mna faida gani katika damu yangu

Nishukapo shimoni?

Mavumbi yatakusifu?

Yataitangaza kweli yako?

10 Zab 4:1 Ee BWANA, usikie, unirehemu,

BWANA, uwe msaidizi wangu.

11 2 Sam 6:14 Uligeuza matanga yangu kuwa machezo;

Ulinivua gunia, ukanivika furaha.

12Ili utukufu wangu ukusifu,

Wala usinyamaze.

Ee BWANA, Mungu wangu,

Nitakushukuru milele.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help