Zab 143 - Swahili Union Version Bible

Sala ya Ukombozi kutoka kwa AduiZaburi ya Daudi.

1Ee BWANA, uisikie sala yangu, uzisikilize dua zangu,

Kwa uaminifu wako unijibu kwa haki yako.

2 Ayu 14:3; 4:17; Mhu 7:20; Rum 3:20; Gal 2:16 Wala usimhukumu mtumishi wako,

Maana kwako hakuna aliye hai mwenye haki.

3 Zab 7:1-2 Maana adui ameifuatia nafsi yangu,

Ameutupa chini uzima wangu.

Amenikalisha mahali penye giza,

Kama watu waliokufa zamani.

4 Zab 61:2 Na roho yangu imezimia ndani yangu,

Moyo wangu ndani yangu umesituka.

5 Zab 77:5,11 Nimezikumbuka siku za kale,

Nimeyatafakari matendo yako yote,

Naziwaza kazi za mikono yako.

6 Zab 28:2 Nakunyoshea mikono yangu;

Nafsi yangu inakuonea kiu kama nchi kame.

7Ee BWANA, unijibu hima, roho yangu imelegea;

Usinifiche uso wako,

Nisifanane nao washukao shimoni

8Unifanye kusikia fadhili zako asubuhi,

Kwa maana nimekutumaini Wewe.

Unijulishe njia nitakayoiendea,

Kwa maana nakuinulia nafsi yangu.

9Ee BWANA, uniponye na adui zangu;

Nimekukimbilia Wewe, unifiche.

10 Zab 25:4; Yn 14:26; Rum 5:5; Efe 4:30; Gal 5:22-23 Unifundishe kuyatenda mapenzi yako,

Kwa maana ndiwe Mungu wangu;

Roho yako mwema aniongoze kwenye nchi sawa,

11Ee BWANA, unihuishe kwa ajili ya jina lako,

Kwa haki yako unitoe roho yangu taabuni;

12Kwa fadhili zako utawakatilia mbali adui zangu;

Na kuwaangamiza wote wanitesao nafsi,

Kwa maana mimi ni mtumishi wako.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help