1 2 Tim 3:1; 2 Pet 3:3; Yud 1:18; 1 Yoh 2:18 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
2kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
3Mwa 9:3; 1 Kor 10:30,31wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.
4Mwa 1:31; Mdo 10:15Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani;
5kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.
Mtumishi Mwema wa Yesu Kristo6Uwakumbushe ndugu mambo hayo, nawe utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, na mzoevu wa maneno ya imani, na mafundisho mazuri yale uliyoyafuata.
71 Tim 1:4; 6:20; 2 Tim 2:16,23; Tit 1:14; 3:9Bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa.
81 Tim 6:6Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.
9 1 Tim 1:15 Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa;
101 Tim 2:3,4kwa maana twajitaabisha na kujitahidi kwa kusudi hili, kwa sababu tunamtumaini Mungu aliye hai, aliye Mwokozi wa watu wote, hasa wa waaminio.
11Mambo hayo uyaagize na kuyafundisha.
12Tit 2:15Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.
13Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika kusoma na kuonya na kufundisha.
141 Tim 5:22; 2 Tim 1:6; Mdo 6:6; 8:17Usiache kuitumia karama ile iliyomo ndani yako, uliyopewa kwa unabii na kwa kuwekewa mikono ya wazee.
15Uyatafakari hayo; ukae katika hayo; ili kuendelea kwako kuwe dhahiri kwa watu wote.
16Rum 11:14Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.