1 Lk 6:6-11; 11:37 Ikawa alipoingia ndani ya nyumba ya mtu mmoja miongoni mwa wakuu wa Mafarisayo siku ya sabato, ale chakula, walikuwa wakimvizia.
2Na tazama, mbele yake palikuwa na mtu mwenye ugonjwa wa safura.
3Yesu akajibu, akawaambia wana-sheria na Mafarisayo, Je! Ni halali kuponya siku ya sabato, ama sivyo?
4Wao wakanyamaza. Akamshika, akamponya, akamruhusu aende zake.
5Mt 12:11; Lk 13:15Akawaambia, Ni nani miongoni mwenu, ikiwa ng’ombe wake au punda wake ametumbukia kisimani, asiyemwopoa mara hiyo siku ya sabato?
6Nao hawakuweza kujibu maneno haya.
Unyenyekevu na Ukarimu7 Mt 23:6 Akawaambia mfano wale walioalikwa, alipoona jinsi walivyochagua viti vya mbele; akisema,
8Mit 25:6-7Ukialikwa na mtu arusini, usiketi katika kiti cha mbele; isiwe kwamba amealikwa mtu mwenye kustahiwa kuliko wewe,
9akaja yule aliyewaalika wewe na yeye, na kukuambia, Mpishe huyu! Ndipo utakapoanza kwa haya kushika mahali pa nyuma.
10Bali ukialikwa, nenda ukaketi mahali pa nyuma, ili ajapo yule aliyekualika akuambie, Rafiki yangu, njoo huku mbele zaidi; ndipo utakapokuwa na utukufu mbele ya wote walioketi pamoja nawe.
11Mt 23:12; Lk 18:14Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.
12Akamwambia na yule aliyemwalika, Ufanyapo chakula cha mchana au cha jioni, usiwaite rafiki zako, wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala jirani zako wenye mali; wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo.
13Kum 14:29Bali ufanyapo karamu waite maskini, vilema, viwete, vipofu,
14Yn 5:29nawe utakuwa heri, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.
Mfano wa Karamu Kuu15 Lk 13:29 Basi aliposikia hayo mmojawapo wa wale walioketi chakulani pamoja naye alimwambia, Heri yule atakayekula mkate katika ufalme wa Mungu.
16Mt 22:2-10Akamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa akaalika watu wengi,
17akamtuma mtumwa wake saa ya chakula awaambie wale walioalikwa, Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari.
18Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame; tafadhali unisamehe.
19Mwingine akasema, Nimenunua ng’ombe jozi tano, ninakwenda kuwajaribu; tafadhali unisamehe.
201 Kor 7:33Mwingine akasema, Nimeoa mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja.
21Yule mtumwa akaenda, akampa bwana wake habari ya mambo hayo. Basi, yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya mji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete.
22Mtumwa akasema, Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa ingaliko nafasi.
23Bwana akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, nyumba yangu ipate kujaa.
24Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu.
Gharama ya Uanafunzi25Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia,
26Mt 10:37,38
Kum 33:9,10; Lk 18:29,30; Yn 12:25Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.27Mt 10:38; 16:24; Mk 8:34; Lk 9:23Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
28Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia?
29Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki,
30wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.
31Au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri, kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na watu elfu ishirini?
32Na kama akiona hawezi, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, mtu yule akali mbali.
33Basi, kadhalika kila mmoja wenu asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
Kuhusu Chumvi34 Mt 5:13; Mk 9:50 Chumvi ni kitu chema; lakini chumvi ikiwa imeharibika, itiwe nini ikolee?
35Haiifai nchi wala jaa; watu huitupa nje. Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.