Zab 141 - Swahili Union Version Bible

Sala ya Kutaka Kulindwa kutoka kwa Uovu

1Ee BWANA, nimekuita, unijie hima,

Uisikie sauti yangu nikuitapo.

2 Efe 5:2; 1 Tim 2:8; Ufu 5:8 Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba,

Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni.

3Ee BWANA, uweke mlinzi kinywani pangu,

Mngojezi mlangoni pa midomo yangu.

4 Mt 6:14; 20:15; Mit 23:6 Usiuelekeze moyo wangu kunako jambo baya,

Nisiyazoelee matendo yasiyofaa,

Pamoja na watu watendao maovu;

Wala nisile vyakula vyao vya anasa.

5Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili;

Anikemee, itakuwa kama mafuta kichwani;

Kichwa changu kisikatae,

Maana siachi kusali kati ya mabaya yao.

6Makadhi wao wakiangushwa kando ya genge,

Watayasikia maneno yangu, maana ni matamu.

7 2 Kor 1:9 Kama kupasua kuni na kuzichanja juu ya nchi,

Ndivyo ilivyo mifupa yetu mdomoni pa kuzimu.

8 Zab 25:15 Macho yangu yanakuelekea Wewe, MUNGU Bwana,

Nimekukimbilia Wewe, usiniache nafsi yangu.

9Unilinde na mtego walionitegea,

Na matanzi yao watendao maovu.

10 Est 7:10; Zab 7:15 Wabaya na waanguke katika nyavu zao wenyewe,

Pindi mimi ninapopita salama.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help