Zab 16 - Swahili Union Version Bible

Wimbo wa Imani na Usalama kwa MunguWimbo wa Daudi.

1 Zab 25:20 Mungu, unihifadhi mimi,

Kwa maana nakukimbilia Wewe.

2Nimemwambia BWANA, Ndiwe BWANA wangu;

Sina wema ila utokao kwako.

3Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora,

Hao ndio niliopendezwa nao.

4Huzuni zao zitaongezeka

Wambadilio Mungu kwa mwingine;

Sitazimimina sadaka zao za damu,

Wala kuyataja majina yao midomoni mwangu.

5BWANA ndiye fungu la posho langu,

Na la kikombe changu;

Wewe unaishika kura yangu.

6Kamba zangu zimeniangukia mahali pema,

Naam, nimepata urithi mzuri.

7Nitamhimidi BWANA aliyenipa shauri,

Naam, mtima wangu umenifundisha usiku.

8 Mdo 2:25-28 Nimemweka BWANA mbele yangu daima,

Kwa kuwa yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa.

9Kwa hiyo moyo wangu unafurahi,

Nao utukufu wangu unashangilia,

Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini.

10 Mdo 13:35; Zab 49:15; Mdo 2:27; Dan 9:24; Lk 1:35 Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu,

Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu.

11 Mdo 2:28 Utanijulisha njia ya uzima;

Mbele za uso wako ziko furaha tele;

Na katika mkono wako wa kuume

Mna mema ya milele.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help