1 nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.
19Yak 2:10; 1 Kor 15:9Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.
20Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
Kuhusu Hasira21 Kut 20:13; 21:12; Law 24:17; Kum 5:17; 17:8 Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu.
221 Yoh 3:15Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.
23Mk 11:25Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,
24iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.
25Mt 6:14,15; 18:35; Lk 12:58,59Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani.
26Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho.
Kuhusu Uzinzi27 Kut 20:14; Kum 5:18 Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;
28Ayu 31:1; 2 Pet 2:14lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
29Mt 18:8,9; Mk 9:42,47; Kol 3:5Jicho lako la kuume likikukosesha, ling’oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
30Mt 18:8; Mk 9:43Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
Kuhusu Talaka31 Kum 24:1-4; Mt 19:7; Mk 10:4 Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka;
32Mt 19:9; Mk 10:11-12; Lk 16:18; 1 Kor 7:10-11lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.
Kuhusu Viapo33 Law 19:12; Hes 30:2; Kum 23:21; Kut 20:7 Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako;
34Yak 5:12; Isa 66:1; Mt 23:16-22; Mdo 7:49lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu;
35Isa 66:1; Zab 48:2wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu.
36Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.
372 Kor 1:17; Yak 5:12Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.
Kuhusu Kujilipiza Kisasi38 Kut 21:24; Law 24:20; Kum 19:21 Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino;
39Lk 6:27-36
Yn 18:22,23; Law 19:18Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili.401 Kor 6:7Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia.
41Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili.
42Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.
Upendo kwa Adui43 Law 19:18 Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;
44Kut 23:4,5; Rum 12:14,20; Lk 23:34; Mdo 7:59lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
45Efe 5:1ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
46Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?
47Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?
48Law 19:2; Kum 18:13Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.