Ebr 1 - Swahili Union Version Bible

Mungu Amenena katika Mwanaye

1Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi,

2Zab 2:8; Yn 1:3; Kol 1:16; Mt 21:38mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.

3Zab 110:1; 2 Kor 4:4; Kol 1:15; Mk 16:19; Ebr 9:14,26Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu;

4Flp 2:9amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao.

Mwana ni Mkuu kuliko Malaika

5 Zab 2:7; 2 Sam 7:14; 1 Nya 17:14; Ebr 5:5; Mdo 13:33 Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote,

Ndiwe mwanangu,

Mimi leo nimekuzaa?

Na tena

Mimi nitakuwa kwake baba,

Na yeye atakuwa kwangu mwana?

6 Kum 32:43; Rum 8:29; Zab 97:7 Hata tena, amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema,

Na wamsujudu malaika wote wa Mungu.

7 Zab 104:4 Na kwa habari za malaika asema,

Afanyaye malaika wake kuwa pepo,

Na watumishi wake kuwa miali ya moto.

8 Zab 45:6-7 Lakini kwa habari za Mwana asema,

Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele;

Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.

9Umependa haki, umechukia maasi;

Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta,

Mafuta ya shangwe kupita wenzio.

10 Zab 102:25-27 Na tena,

Wewe, Bwana, hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi,

Na mbingu ni kazi za mikono yako;

11Hizo zitaharibika, bali wewe unadumu;

Nazo zote zitachakaa kama nguo,

12Na kama mavazi utazizinga, nazo zitabadilika;

Lakini wewe u yeye yule,

Na miaka yako haitakoma.

13 Zab 110:1 Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote,

Uketi mkono wangu wa kuume

Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako?

14 Dan 7:10; Zab 34:8; 91:11 Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help