Zab 91 - Swahili Union Version Bible

Hakikisho la Ulinzi wa Mungu

1Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu

Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.

2Nitasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu,

Mungu wangu nitakayemtumaini.

3Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji,

Na katika tauni iharibuyo.

4 Zab 61:4 Kwa manyoya yake atakufunika,

Chini ya mbawa zake utapata kimbilio;

Uaminifu wake ni ngao na kigao.

5 Ayu 5:19; Mit 3:23; Isa 43:2 Hutaogopa hofu ya usiku,

Wala mshale urukao mchana,

6Wala tauni ipitayo gizani,

Wala uele uharibuo adhuhuri,

7Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako.

Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume!

Hata hivyo hautakukaribia wewe.

8 Mal 1:5 Ila kwa macho yako utatazama,

Na kuyaona malipo ya wasio haki.

9Kwa kuwa Wewe BWANA ndiwe kimbilio langu;

Umemfanya Aliye juu kuwa makao yako.

10 Mit 1:33; 2 The 3:3; 2 Pet 2:9 Mabaya hayatakupata wewe,

Wala tauni haitaikaribia hema yako.

11 Mt 4:6; Lk 4:10 Zab 34:7; Mt 4:6; Lk 4:10; Ebr 1:14 Kwa kuwa atakuagizia malaika zake

Wakulinde katika njia zako zote.

12 Ayu 5:23; Zab 37:24; Mt 4:6; Lk 4:11 Mikononi mwao watakuchukua,

Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

13 Lk 10:19 Utawakanyaga simba na nyoka,

Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu.

14Kwa kuwa amekaza kunipenda

Nitamwokoa; na kumweka palipo juu,

Kwa kuwa amenijua Jina langu.

15 Ayu 22:27; Zab 18:3; Yer 33:3; Zek 13:9; Ebr 5:7; Zab 43:2; 1 Sam 2:30 Ataniita nami nitamwitikia;

Nitakuwa pamoja naye taabuni,

Nitamwokoa na kumtukuza;

16Kwa siku nyingi nitamshibisha,

Nami nitamwonyesha wokovu wangu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help