1BWANA asipoijenga nyumba
Waijengao wafanya kazi bure.
BWANA asipoulinda mji
Yeye aulindaye akesha bure.
2 Mwa 3:17 Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema,
Na kukawia kwenda kulala,
Na kula chakula cha taabu;
Yeye humpa mpenzi wake usingizi.
3 Mwa 33:5; Kum 28:4 Tazama, wana ndio urithi wa BWANA,
Uzao wa tumbo ni thawabu.
4Kama mishale mkononi mwa shujaa,
Ndivyo walivyo wana wa ujanani.
5Heri mtu yule
Aliyelijaza podo lake hivyo.
Naam, hawataona aibu
Wanaposema na adui langoni.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.