1 wakamkusanyikia kikosi kizima.
28Wakamvua nguo, wakamvika vazi jekundu.
29Wakasokota taji ya miiba, wakaiweka juu ya kichwa chake, na mwanzi katika mkono wake wa kuume; wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki, wakisema, Salamu, Mfalme wa Wayahudi!
30Isa 50:6Kisha wakamtemea mate, wakautwaa ule mwanzi, wakampiga-piga kichwani.
31Mk 15:20-41; Lk 23:26,33-49; Yn 19:16-30Walipokwisha kumdhihaki, wakalivua lile vazi, wakamvika mavazi yake, wakamchukua kumsulibisha.
Yesu Asulubiwa32Hata walipokuwa wakitoka, wakamwona mtu Mkirene, jina lake Simoni; huyu wakamshurutisha auchukue msalaba wake.
33Na walipofika mahali paitwapo Golgotha, yaani, Fuvu la kichwa,
34Zab 69:22wakampa kunywa divai iliyochanganyika na nyongo; lakini yeye alipoionja hakutaka kunywa.
35Zab 22:19Walipokwisha kumsulibisha, waligawa mavazi yake, wakipiga kura;
36Wakaketi, wakamlinda huko.
37Wakaweka juu ya kichwa chake mashitaka yake, yaliyoandikwa HUYU NI YESU, MFALME WA WAYAHUDI.
38Isa 53:12Wakati uo huo wanyang’anyi wawili wakasulibiwa pamoja naye, mmoja mkono wake wa kuume, na mmoja mkono wake wa kushoto.
39Zab 22:8; 109:25Nao waliokuwa wakipita njiani wakamtukana, wakitikisa-tikisa vichwa vyao, wakisema,
40Mt 26:61; Yn 2:19Ewe mwenye kulivunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu, jiokoe nafsi yako; ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, shuka msalabani.
41Kadhalika na wale wakuu wa makuhani wakamdhihaki pamoja na waandishi na wazee, wakisema, Aliokoa wengine, hawezi kujiokoa mwenyewe.
42Yeye ni mfalme wa Israeli; na ashuke sasa msalabani, nasi tutamwamini.
43Zab 22:9Amemtegemea Mungu; na amwokoe sasa, kama anamtaka; kwa maana alisema, Mimi ni Mwana wa Mungu.
44Pia wale wanyang’anyi waliosulibiwa pamoja naye walimshutumu vile vile.
Kifo cha Yesu45Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hata saa tisa.
46Zab 22:2Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?
47Na baadhi yao waliohudhuria, waliposikia, walisema, Huyu anamwita Eliya.
48Zab 69:22Mara mmoja wao akaenda mbio, akatwaa sifongo, akaijaza siki, akaitia juu ya mwanzi, akamnywesha.
49Wale wengine wakasema, Acha; na tuone kama Eliya anakuja kumwokoa.
50Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake.
51 Kut 26:31-33; Ebr 10:19,20 Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;
52makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala;
53Mdo 26:23; Dan 12:2nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi.
54Basi yule akida, na hao waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu, walipoliona tetemeko la nchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakisema, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.
55Lk 8:2-3Palikuwa na wanawake wengi pale wakitazama kwa mbali, hao ndio waliomfuata Yesu toka Galilaya, na kumtumikia.
56Mt 20:20Miongoni mwao alikuwamo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo na Yusufu, na mama yao wana wa Zebedayo.
Kuzikwa kwa Yesu57 Mk 15:42-47; Lk 23:50-55; Yn 19:38-42 Kut 34:25 Hata ilipokuwa jioni akafika mtu tajiri wa Arimathaya, jina lake Yusufu, naye mwenyewe alikuwa mwanafunzi wa Yesu;
58mtu huyu alimwendea Pilato akauomba mwili wa Yesu. Ndipo Pilato akaamuru apewe.
59Yusufu akautwaa mwili, akauzonga-zonga katika sanda ya kitani safi,
60Isa 53:9akauweka katika kaburi lake jipya, alilokuwa amelichonga mwambani; akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda zake.
61Na pale walikuwapo Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, wameketi kulielekea kaburi.
Ulinzi katika Kaburi62Hata siku ya pili, ndiyo iliyo baada ya Maandalio, wakuu wa makuhani, na Mafarisayo wakamkusanyikia Pilato,
63Mt 16:21; 27:40; 12:40; 17:23; 20:19; Mk 8:31; 9:31; 10:33-34; Lk 9:22; 18:31-33wakasema, Bwana, tumekumbuka kwamba yule mjanja alisema, alipokuwa akali hai, Baada ya siku tatu nitafufuka.
64Basi amuru kwamba kaburi lilindwe salama hata siku ya tatu; wasije wanafunzi wake wakamwiba, na kuwaambia watu, Amefufuka katika wafu; na udanganyifu wa mwisho utapita ule wa kwanza.
65Pilato akawaambia, Mna askari; nendeni mkalilinde salama kadiri mjuavyo.
66Dan 6:17Wakaenda, wakalilinda kaburi salama, kwa kulitia lile jiwe muhuri, pamoja na wale askari walinzi.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.