Yn 14 - Swahili Union Version Bible

Yesu ni Njia ya kwenda kwa Baba

1 Yn 14:27; Mk 11:22 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.

2Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.

3Yn 12:26; 17:24Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.

4Nami niendako mwaijua njia.

5Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia?

6Ebr 10:20; Mt 11:27; Yn 11:25; Rum 5:1,2Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.

7Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.

8Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha.

9Yn 12:45; Ebr 1:3; Mt 17:17Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?

10Yn 12:49Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake.

11Yn 14:20; Yn 10:25,38Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe.

12Mk 16:19,20Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.

13Yn 15:7; Mk 11:24; 1 Yoh 5:14Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.

14Yn 16:23,24Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.

Ahadi ya kupewa Roho Mtakatifu

15 Yn 15:10; 1 Yoh 5:3 Mkinipenda, mtazishika amri zangu.

16Yn 14:26; 15:26; 16:7; 1 Yoh 2:1Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;

17Yn 7:39; 16:13; Mt 10:20; Rum 8:26ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.

18Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.

19Yn 16:16Bado kitambo kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona. Na kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai.

20Yn 17:21-23Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu.

212 Kor 3:18; 1 Yoh 5:3Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.

22Mdo 10:41Yuda (siye Iskariote), akamwambia, Bwana, imekuwaje ya kwamba wataka kujidhihirisha kwetu, wala si kwa ulimwengu?

23Yn 13:34; 14:21; Mit 8:17; Mt 18:20; 28:20; Efe 3:17; 2 Kor 6:16Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.

24Yn 7:16; 1 Yoh 2:5Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka.

25Hayo ndiyo niliyowaambia wakati nilipokuwa nikikaa kwenu.

26Yn 14:16; Mt 10:19Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.

27Yn 1:16,33; Flp 4:7Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.

28Yn 14:3,6,18; Lk 24:52Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi.

29Yn 13:19Na sasa nimewaambia kabla halijatokea, kusudi litakapotokea mpate kuamini.

30Yn 12:31; Efe 2:2Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu.

31Yn 10:18; Mt 26:46; Mk 14:42Lakini ulimwengu ujue ya kuwa nampenda Baba; na kama vile Baba alivyoniamuru; ndivyo nifanyavyo. Ondokeni, twendeni zetu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help