Zab 146 - Swahili Union Version Bible

Sifa kwa Kupata Msaada wa Mungu

1Haleluya.

Ee nafsi yangu, umsifu BWANA.

2Nitamsifu BWANA muda ninaoishi,

Nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai.

3 Isa 2:22 Msiwatumainie wakuu,

Wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake.

4 Mhu 12:7; 1 Kor 2:6 Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake,

Siku hiyo mawazo yake yapotea.

5 Yer 17:7 Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake,

Na tumaini lake ni kwa BWANA, Mungu wake,

6 Mik 7:20; Mdo 4:24; 14:15; Ufu 14:7 Aliyezifanya mbingu na nchi,

Bahari na vitu vyote vilivyomo.

Huishika kweli milele,

7Huwafanyia hukumu walioonewa,

Huwapa wenye njaa chakula;

BWANA hufungua waliofungwa;

8BWANA huwafumbua macho waliopofuka;

BWANA huwainua walioinama;

BWANA huwapenda wenye haki;

9BWANA huwahifadhi wageni;

Huwategemeza yatima na mjane;

Bali njia ya wasio haki huipotosha.

10BWANA atamiliki milele,

Mungu wako, Ee Sayuni, kizazi hata kizazi.

Haleluya.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help