Zab 140 - Swahili Union Version Bible

Sala ya Ukombozi kutoka kwa AduiKwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

1Ee BWANA, uniokoe na mtu mbaya,

Unihifadhi na mtu wa jeuri.

2Waliowaza mabaya mioyoni mwao,

Kila siku huondokesha vita.

3 Rum 3:13 Wamenoa ndimi zao kama nyoka,

Sumu ya fira i chini ya midomo yao.

4Ee BWANA, unilinde na mikono ya mtu asiye haki;

Unihifadhi na mtu wa jeuri;

Waliowaza kuzipotosha hatua zangu.

5 Zab 10:9; Yer 18:22; Lk 11:53-54 Wenye kiburi wamenifichia mtego na kamba;

Wametandika wavu kando ya njia;

Wameniwekea matanzi.

6 Zab 16:2 Nimemwambia BWANA, Ndiwe Mungu wangu;

Ee BWANA, uisikie sauti ya dua zangu.

7 Kum 33:27-29; Zab 18:32 Ee MUNGU Bwana, nguvu za wokovu wangu,

Umenifunika kichwa changu siku ya vita.

8 Ayu 5:12,13 Ee BWANA, usimpe asiye haki tamaa zake,

Usiifanikishe hila yake, wasije wakajiinua.

9 Zab 7:16 Nao wainuapo vichwa watu wanaonizunguka,

Madhara ya midomo yao yawafunike.

10 Zab 11:6 Makaa ya moto yawaangukie, watupwe motoni,

Na katika mashimo, wasipate kusimama tena.

11Msingiziaji hatawekwa imara katika nchi,

Mtu wa jeuri, uovu humwinda kumwangamiza.

12 Zab 109:31 Najua ya kuwa BWANA atamfanyia mnyonge hukumu,

Na wahitaji haki yao.

13Hakika wenye haki watalishukuru jina lako,

Wenye adili watakaa mahali ulipo Wewe.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help