1 Ayu 16:10; Omb 3:30; Mt 27:30 Sasa utajikusanya vikosi vikosi, Ee binti wa vikosi; yeye amemhusuru; watampiga mwamuzi wa Israeli shavuni mwake kwa fimbo.
2 Mwa 35:19; 49:10; Zab 132:6; Isa 9:6; Zab 90:2; Mit 8:22; Yn 1:1; Mt 2:6; Yn 7:42 Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.
3Kwa sababu hiyo atawatoa, hata wakati wa kuzaa kwake aliye na utungu; ndipo hayo mabaki ya nduguze watawarudia wana wa Israeli.
4Zab 72:8; Isa 52:13; Zek 9:10; Lk 1:32Naye atasimama, na kulisha kundi lake kwa nguvu za BWANA, kwa enzi ya jina la BWANA, Mungu wake; nao watakaa; maana sasa atakuwa mkuu hata miisho ya dunia.
5Isa 9:6; Lk 2:14; Efe 2:14; Kol 1:20Na mtu huyu atakuwa amani yetu; wakati Mwashuri atakapoingia katika nchi yetu, na kuyakanyaga majumba yetu, hapo mtaondokesha wachungaji saba juu yake, na wakuu wanane.
6Lk 1:71; Mwa 10:8-11Nao wataiharibu nchi ya Ashuru kwa upanga, na nchi ya Nimrodi katika malango yake; naye atatuokoa na Mwashuri, atakapoingia katika nchi yetu, na kukanyaga ndani ya mipaka yetu.
Wajibu wa Mabaki7 Zab 110:3 Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya kabila nyingi mfano wa umande utokao kwa BWANA, mfano wa manyunyu katika manyasi; yasiyomngojea mtu, wala kuwakawilia wanadamu.
8Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya mataifa, kati ya kabila nyingi, mfano wa simba kati ya wanyama wa msituni, kama mwana-simba kati ya makundi ya kondoo, ambaye, akiwa anapita katikati, hukanyaga-kanyaga na kurarua-rarua, wala hakuna wa kuokoa.
9Mkono wako na uinuliwe juu ya adui zako, na adui zako wote wakauliwe mbali.
10 Zek 9:10 Kisha itakuwa katika siku hiyo, asema BWANA, nitawakatilia mbali farasi zako watoke kati yako, nami nitayaharibu magari yako ya vita;
11nami nitaikatilia mbali miji ya nchi yako, na ngome zako zote nitaziangusha;
12nami nitakatilia mbali uchawi, usiwe mkononi mwako; wala hutakuwa tena na watu wenye kutabana;
13Zek 13:2; Isa 2:8nami nitakatilia mbali sanamu zako na nguzo zako, zitoke kati yako; wala hutaiabudu tena kazi ya mikono yako.
14Nami nitayang’oa maashera yenu, yasiwe kati yako; nami nitaiangamiza miji yako.
15Nami nitajilipiza kisasi katika hasira na ghadhabu juu ya mataifa wasiosikiliza.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.