2 Petro 1 - Swahili Revised Union Version DC

Salamu

1Simoni Petro, mtumwa na mtume wa Yesu Kristo, kwa wale waliopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika hali ya Mungu wetu, na Mwokozi Yesu Kristo.

2 hii, kuwaamsha kwa kuwakumbusha.

14Yn 21:18,19 Nikijua kwamba kule kuwekea mbali maskani yangu kwaja upesi, kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyonionesha.

15Lakini nitajitahidi, ili kila wakati baada ya kufariki kwangu mpate kuyakumbuka mambo hayo.

Mashahidi wa utukufu wa Kristo

16Maana hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, tulipowajulisha ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake; bali tulikuwa tumeuona wenyewe ukuu wake.

17Mt 17:1-5; Mk 9:2-7; Lk 9:28-35 Maana alipata heshima na utukufu kutoka kwa Mungu Baba hapo alipoletewa sauti iliyotoka katika utukufu mkuu, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.

18Na sauti hiyo sisi tuliisikia ikitoka mbinguni tulipokuwa pamoja naye katika mlima ule mtakatifu.

19Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa iangazayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.

20Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika Maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.

212 Tim 3:16,17 Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help