Zaburi 48 - Swahili Revised Union Version DC

Utukufu wa nguvu za SayuniWimbo. Zaburi ya Wakorahi.

1 Isa 2:2; Oba 1:17; Mik 4:1 Bwana ndiye aliye mkuu,

Na mwenye kusifiwa sana.

Katika mji wa Mungu wetu,

Katika mlima wake mtakatifu.

2 Mt 5:35; Yer 3:19; Omb 2:15; Eze 20:6; Isa 14:13 Kuinuka kwake ni mzuri sana,

Ni furaha ya dunia yote.

Mlima Sayuni, kule upande wa kaskazini,

Mji wa Mfalme mkuu.

3Mungu katika majumba yake

Amejijulisha kuwa ngome.

4 2 Sam 10:6 Maana, tazama, wafalme walikusanyika;

Walikuja wote pamoja.

5Mara Walipouona, wakashtuka;

Wakafadhaika na kukimbia.

6Papo hapo tetemeko liliwashika,

Uchungu kama wa mwanamke azaaye.

7 Eze 27:26 Kama upepo wa mashariki

Unapovunja jahazi za Tarshishi.

8 Isa 2:2; Mik 4:1 Kama tulivyosikia, ndivyo tulivyoona,

Katika mji wa BWANA wa majeshi.

Mji wa Mungu wetu;

Mungu atauimarisha hata milele.

9Tumezitafakari fadhili zako, Ee Mungu,

Katikati ya hekalu lako.

10 Mal 1:11 Kama lilivyo jina lako, Ee Mungu,

Ndivyo na sifa yako hadi miisho ya dunia.

Mkono wako wa kulia umejaa haki;

11Na ufurahi mlima Sayuni.

Binti za Yuda na washangilie

Kwa sababu ya hukumu zako.

12Tembeeni katika Sayuni,

Uzungukeni mji wote,

Ihesabuni minara yake,

13Tieni moyoni boma zake,

Yafikirini majumba yake,

Mpate kuwaambia kizazi kitakachokuja.

14 Isa 25:9 Kwa maana ndivyo alivyo

MUNGU, Mungu wetu.

Milele na milele

Yeye ndiye atakayetuongoza.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help