1 Yer 2:21; Zab 80:8 Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.
2Mt 15:13 Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.
3Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.
4Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi hamuwezi, msipokaa ndani yangu.
51 Kor 12:12,27; 2 Kor 3:5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamuwezi kufanya neno lolote.
6Mt 3:10; 13:40 Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea.
7Mk 11:24 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lolote mtakalo nanyi mtatendewa.
8Mt 5:16 Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.
9Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu.
10Yn 8:29; 14:15; 1 Yoh 2:4,8 Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.
11Yn 17:13 Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe.
12Yn 13:34; 15:17; 1 Yoh 3:11,23; 2 Yoh 1:5; Mk 12:30 Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi.
13Yn 10:12; 1 Yoh 3:16 Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.
14Yn 8:31; Mt 12:50; 28:20 Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo.
15Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu.
16Yn 6:70; 13:18 Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lolote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.
17Haya nawaamuru ninyi, mpate kupendana.
Chuki ya ulimwengu18 Yn 7:7; 1 Yoh 3:13 Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi.
191 Yoh 4:5; Yn 17:14; Lk 6:22 Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi niliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia.
20Mt 10:24; Lk 6:40; Yn 13:16 Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu.
21Yn 10:22; 16:3; Mt 5:11; Mk 13:13 Lakini haya yote watawatenda kwa ajili ya jina langu, kwa kuwa hawamjui yeye aliyenituma.
22Kama nisingalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa hawana kisingizio kwa dhambi yao.
23Yn 5:23; 1 Yoh 2:23; Lk 10:16 Yeye anichukiaye mimi humchukia na Baba yangu.
24Yn 14:11 Kama nisingalitenda kwao kazi asizozitenda mtu mwingine, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa wametuona mimi na Baba yangu, na kutuchukia.
25Zab 35:19; 69:4 Lakini litimie lile neno lililoandikwa katika torati yao, Walinichukia bure.
26Yn 14:26; Lk 24:49 Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia.
27Lk 1:2; Mdo 1:8; 5:32 Nanyi pia mnashuhudia, kwa kuwa tangu mwanzo mmekuwapo pamoja nami.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.