1Ee Mungu, ukisikie kilio changu,
Uyasikilize maombi yangu.
2 1 Tim 2:8 Toka mwisho wa nchi nitakulilia ninapozimia moyo,
Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda.
3 Mit 18:10 Kwa maana ulikuwa kimbilio langu,
Ngome yenye nguvu adui asinipate.
4 Zab 15:1; 23:6; Ufu 3:12 Nitakaa katika hema yako milele,
Na kupata kimbilio chini ya mbawa zako.
5 1 Kor 3:21-23 Maana Wewe, Mungu, umezisikia nadhiri zangu.
Umewapa urithi wao waliogopao jina lako.
6Utaziongeza siku za mfalme,
Miaka yake itakuwa kama vizazi vingi.
7 Zab 41:12; Lk 1:32 Atakaa mbele za Mungu milele,
Ziagize fadhili na kweli zimhifadhi.
8 Zab 56:12 Ndivyo nitakavyoliimbia jina lako daima,
Ili niondoe nadhiri zangu kila siku.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.