Mithali 14 - Swahili Revised Union Version DC

1 Rut 4:11; Mit 24:3,4 Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake;

Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.

2 Ayu 12:4 Yeye aendaye kwa unyofu wake humcha BWANA;

Bali aliye mkaidi katika njia zake humdharau.

3 Mit 12:6 Katika kinywa cha mpumbavu mna fimbo ya kiburi,

Bali midomo ya wenye hekima huwahifadhi.

4Zizi ni safi ambapo hapana ng'ombe;

Bali nguvu za ng'ombe zaleta faida nyingi.

5 Kut 20:16 Shahidi mwaminifu hatasema uongo;

Bali shahidi wa uongo, pumzi zake ni uongo.

6 Mit 17:24 Mwenye dharau hutafuta hekima, asiipate;

Bali maarifa huwa mepesi kwa mwenye ufahamu.

7Toka mbele ya uso wa mpumbavu,

Maana hutaona kwake midomo ya maarifa.

8 Lk 12:20; 1 Kor 3:19 Akili za mwenye busara ni kujua njia yake;

Lakini upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu.

9 Mit 1:22 Wapumbavu huidharau hatia;

Bali upo upendeleo kwa wenye haki.

10Moyo huujua uchungu wa nafsi yake,

Wala mgeni haishiriki furaha yake.

11 Ayu 8:15; Mit 3:33 Nyumba ya mtu mwovu itabomolewa;

Bali hema la mwenye haki litafanikiwa.

12 Mit 16:25; Rum 6:21 Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu,

Lakini mwisho wake ni njia za mauti.

13 Mhu 2:2 Hata wakati wa kucheka moyo huwa na huzuni;

Na mwisho wa furaha ni uzito wa moyo.

14 Mit 12:14; 2 Kor 1:12; Flp 4:7 Ageukaye moyoni hushiba njia zake mwenyewe;

Na mtu mwema ataridhika nafsini mwake.

15Mjinga huamini kila neno;

Bali mwenye busara huangalia sana aendavyo.

16 Mit 22:3 Mwenye hekima huhadhari, na kujitenga na uovu;

Bali mpumbavu hupuuza yote, na hajali.

17Yeye aonaye hasira upesi atatenda kwa ujinga;

Na mtu mwenye hila mbaya huzirwa.

18Wajinga hurithi upumbavu;

Bali wenye busara huvikwa taji la maarifa.

19Wabaya huinama mbele ya wema,

Na wasio haki malangoni mwao wenye haki.

20 Mit 19:7 Maskini huchukiwa hata na jirani yake;

Bali tajiri ana marafiki wengi.

21 Zab 41:1 Amdharauye mwenzake afanya dhambi;

Bali amhurumiaye maskini ana heri.

22Je! Hawakosi wawazao mabaya?

Bali fadhili na kweli zina wao wawazao mema.

23Katika kila kazi mna faida;

Bali maneno ya midomo huleta hasara tu.

24Taji la wenye hekima ni mali zao;

Bali upumbavu wa wajinga ni upumbavu tu.

25Shahidi wa kweli huponya nafsi za watu;

Bali atoaye uongo hudanganya.

26Kumcha BWANA ni tumaini imara;

Watoto wake watakuwa na kimbilio.

27 Mit 13:14 Kumcha BWANA ni chemchemi ya uzima,

Ili kuepukana na tanzi za mauti.

28Utukufu wa mfalme ni wingi wa watu wake;

Bali uchache wa watu ni uharibifu wa mkuu wao.

29 Mit 15:18; Mt 11:29; 1 Kor 13:4,5; Yak 1:19 Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi;

Bali mwenye roho ya hamaki hutukuza upumbavu.

30 Ayu 5:2; Zab 112:10; Mdo 7:9; Rum 1:29; Yak 4:5 Moyo ulio mzima ni uhai wa mwili;

Bali husuda ni ubovu wa mifupa.

31 Ayu 31:15,16; Mhu 5:8; Mit 17:5; 22:2; Mt 25:40; 1 Yoh 3:17 Amwoneaye maskini humsuta Muumba wake;

Bali yeye awahurumiaye wahitaji humheshimu.

32 Ayu 13:15; Zab 23:4; 2 Kor 1:9; 2 Tim 4:18 Mtu mbaya husukumwa chini katika kutenda mabaya kwake;

Bali mwenye haki ana matumaini katika kufa kwake.

33Hekima hukaa katika moyo wake mwenye ufahamu;

Bali yaliyo ndani ya wapumbavu hudhihirika.

34Haki huinua taifa;

Bali dhambi ni aibu ya watu wowote.

35 Mt 24:45-47 Upendeleo wa mfalme humwelekea mtumwa atendaye kwa busara;

Bali hasira yake itakuwa juu yake aletaye aibu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help