Mwanzo 35 - Swahili Revised Union Version DC

Yakobo arudi Betheli

1

9

12Mwa 12:7; 13:15; 28:13; Kut 32:13 Na nchi hii niliyowapa Abrahamu na Isaka nitakupa wewe, na uzao wako baada yako nitawapa nchi hiyo.

13Mwa 17:22 Mungu akakwea juu kutoka kwake mahali hapo aliposema naye.

14Mwa 28:18-19 Yakobo akasimamisha nguzo mahali aliposema naye, nguzo ya mawe, akamimina juu yake sadaka ya kinywaji, akamimina mafuta juu yake.

15Yakobo akapaita mahali pale, Mungu aliposema naye, Betheli.

Kuzaliwa kwa Benyamini na kufa kwa Raheli

16Wakasafiri kutoka Betheli, na kabla ya kufika Efrata, Raheli akashikwa na uchungu wa kuzaa, na uchungu wake ulikuwa mkali.

17Mwa 30:24 Ikawa alipokuwa anashikwa sana na uchungu, mkunga akamwambia, Usiogope, maana sasa utamzaa mwanamume mwingine.

18Ikawa hapo katika kutoa roho yake, maana alikufa, akamwita jina lake Benoni, lakini babaye alimwita Benyamini.

19Mwa 48:7; Rut 1:2; 4:11; Mik 5:2; Mt 2:6 Akafa Raheli, akazikwa katika njia ya Efrata, ndio Bethlehemu.

201 Sam 10:2 Yakobo akasimamisha nguzo juu ya kaburi lake, ndiyo nguzo ya kaburi la Raheli hata leo.

21Mik 4:8 Kisha akasafiri Israeli akapiga hema yake upande wa pili wa mnara wa Ederi.

22Mwa 49:4; 1 Nya 5:1 Ikawa Israeli alipokuwa akikaa katika nchi ile, Reubeni akaenda akalala na Bilha, suria wa babaye; Israeli akasikia habari.

Basi hao wana wa Yakobo walikuwa kumi na wawili.

23Mwa 46:8; Kut 1:2 Wana wa Lea ni Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, na Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni.

24Wana wa Raheli, ni Yusufu na Benyamini.

25Wana wa Bilha, kijakazi wa Raheli, ni Dani na Naftali.

26Wana wa Zilpa, kijakazi wa Lea, ni Gadi na Asheri. Hawa ndio wana wa Yakobo aliozaliwa katika Padan-aramu.

Kufa kwa Isaka

27 Mwa 13:18; Yos 14:15 Yakobo akaja kwa Isaka, babaye, huko Mamre, mji wa Arba, ndio Hebroni, walipokaa ugenini Abrahamu na Isaka.

28Siku za Isaka zilikuwa miaka mia moja na themanini.

29Mhu 12:7; Mwa 15:15; 25:8,9; 49:31 Naye Isaka akakata roho, akafa, akakusanyika kwa watu wake, ni mzee, ameshiba siku. Esau na Yakobo, wanawe, wakamzika.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help