1Laiti ungepasua mbingu, na kushuka, ili milima itetemeke mbele zako;
2kama vile moto uchomapo vichaka, na moto uchemshapo maji; ili kuwajulisha adui zako jina lako, mataifa wakatetemeke mbele zako!
3Ulipofanya mambo ya kutisha tusiyoyatazamia, ulishuka, milima ikatetemeka mbele zako.
4Zab 31:19; Kol 1:26,27; 1 Tim 3:16; Ufu 21:1-4; 1 Kor 2:9,10 Maana tangu zamani za kale watu hawakusikia, wala kufahamu kwa masikio, wala jicho halikuona Mungu, ila wewe, atendaye mambo kwa ajili yake amngojaye.
5Mdo 10:35; Mal 3:6 Wewe wamlaki yeye afurahiaye yaliyo haki na kuyatenda, watu wale wakukumbukao katika njia zako; tazama, ulikuwa na hasira, nasi tulitenda dhambi; tumekuwa katika dhambi kwa muda mrefu, nasi Je! Tutaokolewa?
6Flp 3:9 Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi; sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa, kama upepo uondoavyo.
7Hos 7:7 Tena hapana aliitiaye jina lako, ajitahidiye akushike; kwa kuwa umetuficha uso wako, nawe umetukomesha kwa njia ya maovu yetu.
8Yer 18:6; Efe 2:10 Lakini sasa, Ee BWANA, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako.
9Ee BWANA, usione hasira nyingi, wala usiukumbuke uovu siku zote; tazama, angalia, twakusihi, sisi sote tu watu wako.
10Miji yako mitakatifu imekuwa jangwa, Sayuni umekuwa jangwa, Yerusalemu umekuwa ukiwa.
112 Fal 25:9; Zab 74:7; Eze 24:21 Nyumba yetu takatifu, nzuri, walimokusifu baba zetu, imeteketea moto; vitu vyetu vyote vyenye kupendeza vimeharibika.
12Utajizuia usiyaangalie mambo haya, Ee BWANA? Utanyamaza, na kutuadhibu vikali?
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.