Zaburi 116 - Swahili Revised Union Version DC

Shukrani kwa kuponywa maradhi

1Haleluya.

Nampenda BWANA kwa kuwa anaisikiliza

Sauti yangu na dua zangu.

2Kwa maana amenitegea sikio lake,

Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote.

3Kamba za mauti zilinizunguka,

Shida za kuzimu zilinipata.

Nilipata dhiki na mateso;

4Nikaliitia jina la BWANA.

Ee BWANA, nakuomba sana,

Uniokoe nafsi yangu.

5 Ezr 9:15; Neh 9:8; Zab 11:7; Yer 12:1; Omb 1:18; Ufu 16:5 BWANA ni mwenye neema na haki,

Naam, Mungu wetu ni mwenye rehema.

6BWANA huwalinda wasio na hila;

Nilidhilika, akaniokoa.

7 Yer 6:16; Mt 11:29 Ee nafsi yangu, urudi pumzikoni mwako,

Kwa kuwa BWANA amekutendea ukarimu.

8Maana umeniponya nafsi yangu na mauti,

Macho yangu na machozi,

Na miguu yangu na kuanguka.

9Nitaenenda mbele za BWANA

Katika nchi za walio hai.

10 2 Kor 4:13 Nilidumisha imani yangu, hata niliposema,

Mimi nateseka sana.

11 2 Fal 4:16; Yer 9:5; Rum 3:4 Nikiwa katika hangaiko langu nikasema,

Wanadamu wote ni waongo.

12Nimrudishie BWANA nini

Kwa ukarimu wake wote alionitendea?

13Nitakipokea kikombe cha wokovu;

Na kulitangaza jina la BWANA;

14 Zab 22:25; Yon 2:6 Nitaziondoa nadhiri zangu kwa BWANA,

Naam, mbele ya watu wake wote.

15 Ayu 5:26; Zab 72:14; Lk 16:22; Ufu 14:13 Kifo cha waaminifu wa Mungu,

kina thamani machoni pa BWANA.

16Ee BWANA, hakika mimi ni mtumishi wako,

Mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako,

Umevifungua vifungo vyangu.

17Nitakutolea dhabihu ya kushukuru;

Na kulitangaza jina la BWANA;

18Nitaziondoa nadhiri zangu kwa BWANA,

Naam, mbele ya watu wake wote.

19Katika nyua za nyumba ya BWANA,

Ndani yako, Ee Yerusalemu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help