Mathayo 10 - Swahili Revised Union Version DC

Wanafunzi kumi na wawili

1 Mk 6:7-13; Lk 9:1-5 Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.

2 Mk 3:14-19; Lk 6:13-16; Yn 1:40-49 Na majina ya hao mitume kumi na wawili ni haya; Wa kwanza Simoni aliyeitwa Petro, na Andrea nduguye; Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye;

3Filipo, na Bartholomayo; Tomaso, na Mathayo mtoza ushuru; Yakobo wa Alfayo, na Thadayo;

4Simoni Mkananayo, na Yuda Iskarioti, naye ndiye aliyemsaliti.

Wajibu wa hao kumi na wawili

5Hao Kumi na Wawili Yesu aliwatuma, akawaagiza, akisema, Katika njia ya Mataifa msiende, wala katika mji wowote wa Wasamaria msiingie.

6Mt 15:24; Mdo 13:46; Yer 50:6 Bali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.

7Lk 10:4-12 Na katika kuenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia.Mt 4:17; Lk 10:9

8Mdo 20:33 Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.

9Msichukue dhahabu, wala fedha, wala pesa mishipini mwenu;

101 Kor 9:14; 1 Tim 5:18; Lk 10:4; Hes 18:31 wala mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo; maana mfanyakazi astahili posho yake.

11Na mji wowote au kijiji chochote mtakachoingia, tafuteni ni nani humo aliye mtu mwaminifu; mkae kwake hadi mtakapotoka.

12Lk 10:5,6 Nanyi mkiingia katika nyumba isalimuni.

13Na nyumba ile ikistahili, amani yenu na iifikie; la, kwamba haistahili, amani yenu na iwarudie ninyi.

14Mdo 13:51; 18:6; Lk 10:10-12 Na mtu asipowakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kung'uteni mavumbi ya miguuni mwenu.

15Mt 11:24; Mwa 19:24-28; Lk 20:47 Amin, nawaambia, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma na Gomora kustahimili adhabu ya siku ya hukumu, kuliko mji ule.

Mateso yajayo

16 Lk 10:3; Yn 10:12; Mdo 20:29; Rum 16:19; Efe 5:15 Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwamwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.

17Mk 13:9-11; Lk 12:11-12; 21:12-15 Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka mabarazani, na katika masinagogi yao watawapiga;Mt 24:9

18Mt 24:14; Mdo 25:23; 27:24 nanyi mtachukuliwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa.

19Lk 12:11,12 Lakini hapo watakapowapeleka, msifikirifikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema.

20Yn 14:26; 1 Kor 2:4 Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu.

21Mk 13:12; Lk 21:16; Mt 10:35; Mik 7:6 Na ndugu atamsaliti nduguye ili auawe, na baba atamsaliti mwana, na wana watawainukia wazazi wao, na kuwaua.

22Mt 24:9,13; Mk 13:13; Lk 21:17; Yn 15:21 Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.

23Mt 16:28 Lakini watakapowafukuza katika mji huu, kimbilieni mwingine; kwa maana ni kweli nawaambia, Hamtaimaliza miji ya Israeli, hata ajapo Mwana wa Adamu.

24 Lk 6:40; Yn 13:16; 15:20 Mwanafunzi hampiti mwalimu wake, wala mtumwa hampiti bwana wake.

25Mt 9:34; 12:24; Mk 3:22; Lk 11:15 Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumwa kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebuli, je! Si zaidi wale walio wa nyumbani mwake?

Astahiliye kuogopewa

26 Lk 12:2-9 Basi, msiwaogope, kwa maana hakuna neno lililositirika, ambalo halitafunuliwa; wala lililofichwa, ambalo halitajulikana.Mk 4:22; Lk 8:17

27Niwaambialo ninyi katika giza, lisemeni katika nuru; na msikialo kwa siri, lihubirini juu ya nyumba.

28Yak 4:12 Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika Jehanamu.

29Je! Mashomoro wawili hawauzwi kwa senti moja? Wala hata mmoja haanguki chini asipojua Baba yenu;

30lakini ninyi, hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote.

31Mt 12:12 Msiogope basi; bora ninyi kuliko mashomoro wengi.

32Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni.

332 Tim 2:12; Lk 9:26 Bali mtu yeyote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.

Si Amani, bali upanga

34 Lk 12:51-53 Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga.

35Mik 7:6 Kwa maana nilikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu;

36na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake.

37Kum 33:9; Lk 14:26,27 Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.

38Mt 16:24; Mk 8:34; Lk 9:23 Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili.

39Mt 16:25; Mk 8:35; Lk 9:24; 17:33; Yn 12:25 Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona.

Thawabu

40 Mk 9:37; Lk 9:48; 10:16; Yn 12:44; 13:20; Mt 18:5 Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma.

41Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; naye ampokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki.

42Mt 25:40; Mk 9:41 Na mtu awaye yote atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa angaa kikombe cha maji baridi, kwa kuwa ni mwanafunzi, amin, nawaambia, haitampotea kamwe thawabu yake.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help