Zaburi 63 - Swahili Revised Union Version DC

Faraja na uhakikisho katika BwanaZaburi ya Daudi, alipokuwa katika Jangwa la Yudea.

1 1 Sam 23:14 Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema,

Nafsi yangu inakuonea kiu,

Mwili wangu wakuonea shauku,

Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji.

2 1 Nya 16:11 Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu,

Nizione nguvu zako na utukufu wako.

3 Yn 3:16 Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai;

Midomo yangu itakusifu.

4Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai;

Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.

5 Zab 17:15; Isa 25:6 Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono;

Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.

6 Zab 149:5 Ninapokukumbuka kitandani mwangu,

Ninakutafakari usiku kucha.

7 2 Kor 1:10 Maana Wewe umekuwa msaada wangu,

Na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia.

8 Isa 26:9 Nafsi yangu inaambatana nawe sana;

Mkono wako wa kulia unanitegemeza.

9Bali waitafutao nafsi yangu, ili kuiangamiza,

Wataingia katika vilindi vya nchi.

10Watatolewa wafe kwa nguvu za upanga,

Watakuwa riziki za mbwamwitu.

11 Sef 1:5 Bali mfalme atamfurahia Mungu,

Kila aapaye kwa Yeye atashangilia,

Kwa maana vinywa vya waongo vitafumbwa.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help