Zaburi 112 - Swahili Revised Union Version DC

Baraka za mwenye haki

1Haleluya.

Heri mtu yule amchaye BWANA,

Apendezwaye sana na maagizo yake.

2Wazawa wake watakuwa hodari duniani;

Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa.

3 Mit 3:16; 15:6; Isa 33:6; Mt 6:33; 2 Kor 6:10 Nyumbani mwake mna utajiri na mali,

Na haki yake yadumu milele.

4Nuru huwaangaza wenye adili gizani;

Ana fadhili na huruma na haki.

5 Lk 6:35 Heri atendaye fadhili na kukopesha;

Atengenezaye mambo yake kwa haki.

6Kwa maana hataondoshwa kamwe;

Mwenye haki atakumbukwa milele.

7Hataogopa habari mbaya;

Moyo wake u imara ukimtumainia BWANA.

8Moyo wake umethibitika hataogopa,

Hata awaone watesi wake wameshindwa.

9 Lk 11:41; Rum 12:13; Mdo 4:35; 20:35; 2 Kor 8:9; 9:9; 1 Tim 6:18 Ametoa kwa ukarimu, na kuwapa maskini,

Haki yake yakaa milele,

Pembe yake itatukuzwa kwa utukufu.

10 Lk 13:28 Asiye haki ataona na kusikitika,

Atasaga meno yake na kuondoka,

Matumaini ya wasio haki hupotea.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help