Zaburi 86 - Swahili Revised Union Version DC

Maombi ya kutaka msaada juu ya watesiSala ya Daudi

1Ee BWANA, utege sikio lako unijibu,

Maana mimi ni maskini na mhitaji.

2Unihifadhi nafsi yangu,

Maana mimi ni mcha Mungu.

Wewe uliye Mungu wangu,

Umwokoe mtumishi wako anayekutumaini.

3Wewe, Bwana, unifadhili,

Maana nakulilia Wewe mchana kutwa.

4Uifurahishe nafsi ya mtumishi wako,

Maana nafsi yangu nakuinulia Wewe, Bwana.

5 Zab 130:7-8; Yoe 2:13 Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema,

Umekuwa tayari kusamehe,

Na mwingi wa fadhili,

Kwa watu wote wakuitao.

6Ee BWANA, uyasikie maombi yangu;

Uisikilize sauti ya dua zangu.

7Siku ya mateso yangu nitakuita,

Kwa maana utaniitikia.

8 Kut 15:11; Kum 3:24; 1 Sam 2:2; 2 Sam 7:22; 1 Fal 8:23 Katikati ya miungu hakuna kama Wewe, Bwana,

Wala matendo mfano wa matendo yako.

9 Zab 95:6-7; Isa 43:7; Ufu 15:4 Mataifa yote uliyoyaumba watakuja;

Watakusujudia Wewe, Bwana,

Watalitukuza jina lako;

10 Kum 6:4; Isa 37:16; Mk 12:29; 1 Kor 8:4; Efe 4:6 Kwa kuwa ndiwe uliye mkuu,

Wewe ndiwe mfanya miujiza,

Ndiwe Mungu peke yako.

11Ee BWANA, unifundishe njia yako;

Nitakwenda katika kweli yako;

Moyo wangu na ufurahi kulicha jina lako;

12Nitakusifu Wewe, Ee Bwana, Mungu wangu,

Kwa moyo wangu wote,

Nitalitukuza jina lako milele.

13 Zab 56:13 Maana fadhili zako kwangu ni nyingi sana;

Umeiopoa nafsi yangu na kuzimu.

14Ee Mungu, wenye kiburi wamenishambulia;

Kundi la watu wakatili wanataka kuniua.

Wala hawakukuweka Wewe

Mbele ya macho yao.

15 Kut 34:6; Hes 14:18; Neh 9:17; Yoe 2:13; Zab 103:8; 111:4 Lakini Wewe, Bwana,

U Mungu wa rehema na neema,

Mvumilivu, mwingi wa fadhili na kweli.

16Unielekee na kunifadhili mimi;

Mpe mtumishi wako nguvu zako,

Umwokoe mwana wa mjakazi wako.

17Unifanyie ishara ya wema,

Wanichukiao waione na kuaibishwa.

Kwa kuwa Wewe, BWANA,

Umenisaidia na kunifariji.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help