1 Zab 4:6; 31:16; 119:135; Hes 6:25,26; 2 Kor 4:6 Mungu na atufadhili na kutubariki,
Na kutuangazia uso wake.
2 Mdo 13:10; Tit 2:11; Lk 2:30-32 Njia yake ijulikane duniani,
Wokovu wake katikati ya mataifa yote.
3 Isa 24:15,16 Watu na wakushukuru, Ee Mungu,
Watu wote na wakushukuru.
4 Zab 96:10 Mataifa na washangilie,
Naam, waimbe kwa furaha,
Maana kwa haki utawahukumu watu,
Na kuwaongoza mataifa walioko duniani.
5Watu na wakushukuru, Ee Mungu,
Watu wote na wakushukuru.
6 Law 26:4; Isa 1:19; Zab 85:9-12 Nchi imetoa mazao yake
MUNGU, Mungu wetu, ametubariki.
7 Zab 22:27 Mungu atatubariki sisi;
Miisho yote ya dunia itamcha Yeye.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.