1Heri kila mtu amchaye BWANA,
Aendaye katika njia yake.
2 Isa 3:10 Taabu ya mikono yako hakika utaila;
Utakuwa heri, na kwako kwema.
3Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao,
Katika nyumba yako.
Wanao watakuwa kama miche ya mizeituni
Wakiizunguka meza yako.
4Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye BWANA.
5 Zab 134:3 BWANA akubariki toka Sayuni;
Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako;
6 Mwa 50:23 Naam, ukawaone wana wa wanao.
Amani ikae na Israeli.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.