1 Zab 25:20 Mungu, unihifadhi mimi,
Kwa maana nakukimbilia Wewe.
2Nimemwambia BWANA, Ndiwe BWANA wangu;
Sina wema ila utokao kwako.
3Nao watakatifu waliopo duniani, ndio Walio bora,
Hao ndio niliopendezwa nao.
4Huzuni zao zitaongezeka
Wambadilio Mungu kwa mwingine;
Sitazimimina sadaka zao za damu,
Wala kuyataja majina yao midomoni mwangu.
5BWANA ndiye fungu la posho langu,
Na la kikombe changu;
Wewe unayaamua maisha yangu.
6Mipaka yangu imeangukia mahali pema,
Naam, nimepata urithi mzuri.
7Nitamhimidi BWANA aniongozaye,
Wakati wa usiku pia moyo wangu hunishauri.
8 Mdo 2:25-28 Nimemweka BWANA mbele yangu daima,
Kwa kuwa yuko kuliani mwangu, sitaondoshwa.
9Kwa hiyo moyo wangu unafurahi,
Nayo nafsi yangu inashangilia,
Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini.
10 Mdo 13:35; Zab 49:15; Mdo 2:27; Dan 9:24; Lk 1:35 Maana hutaitupa kuzimu nafsi yangu,
Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu.
11 Mdo 2:28 Utanijulisha njia ya uzima;
Mbele za uso wako kuna furaha tele;
Na katika mkono wako wa kulia
Mna mema ya milele.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.