1 bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki.
Huyu ndiye Kristo?25 Yn 7:19 Basi baadhi ya watu wa Yerusalemu wakasema, Je! Huyu siye wanayemtafuta ili wamwue?
26Na kumbe! Anena waziwazi, wala hawamwambii neno! Inawezekana hao wakuu wanajua hakika ya kuwa huyu ndiye Kristo?
27Yn 7:41 Lakini huyu twamjua atokako; bali Kristo atakapokuja hakuna ajuaye atokako.
28Basi Yesu akapaza sauti yake hekaluni, akifundisha na kusema, Mimi mnanijua, na huko nitokako mnakujua; wala sikuja kwa nafsi yangu; ila yeye aliyenituma ni wa kweli, msiyemjua ninyi.
29Mt 11:27 Mimi namjua, kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma.
30Yn 8:20; 13:1; Lk 22:53 Basi wakatafuta kumkamata; lakini hakuna mtu aliyeunyosha mkono wake ili kumshika, kwa sababu saa yake ilikuwa haijafika bado.
31Yn 8:30; 10:42; 11:45; 12:42 Na watu wengi katika mkutano wakamwamini; wakasema, Atakapokuja Kristo, je! Atafanya ishara nyingi zaidi kuliko hizi alizozifanya huyu?
Maofisa watumwa kumkamata Yesu32Mafarisayo wakawasikia mkutano wakinung'unika hivi juu yake; basi wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakatuma watumishi ili wamkamate.
33 Yn 13:33 Basi Yesu akasema, Bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; kisha naenda zangu kwake yeye aliyenituma.
34Yn 8:21; 13:36; 17:24 Mtanitafuta wala hamtaniona; nami nilipo ninyi hamwezi kuja.
35Basi Wayahudi wakasemezana, Huyu atakwenda wapi hata sisi tusimwone? Ati! Atakwenda kwa Utawanyiko wa Wagiriki, na kuwafundisha Wagiriki?
36Ni neno gani hilo alilolisema, Mtanitafuta wala hamtaniona; nami nilipo ninyi hamwezi kuja?
Mito ya maji yaliyo hai37 Law 23:36; Yn 4:10,14 Katika siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe.
38Eze 47:1,12; Zek 13:1; 14:8; Yoe 2:28; 3:18; Isa 44:3; 55:1; 58:11 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.
39Yn 16:7; 2 Kor 3:17 Na neno hilo alilisema kuhusu Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa.
Mgawanyiko kati ya watu40 Yn 6:14; Kum 18:15 Basi wengine katika mkutano walipoyasikia maneno hayo, walisema, Hakika huyu ndiye nabii yule.
41Yn 1:46 Wengine walisema, Huyu ndiye Kristo. Wengine wakasema, Je! Kristo atoka Galilaya?
422 Sam 7:12; Mik 5:2; Mt 2:5,6; 22:42; Zab 89:3 Andiko halikusema ya kwamba Kristo atoka katika uzao wa Daudi, na kutoka Bethlehemu, mji ule alioukaa Daudi?
43Yn 9:16 Basi kukaingia matengano katika mkutano kwa ajili yake.
44Yn 7:30 Baadhi yao wakataka kumkamata, lakini hakuna mtu aliyenyosha mikono yake ili kumshika.
Kutoamini kwa wenye mamlaka45 Yn 7:32 Basi wale watumishi wakawaendea wakuu wa makuhani na Mafarisayo. Nao wakawaambia, Mbona hamkumleta?
46Mt 7:28,29 Wale watumishi wakajibu. Hajanena kamwe mtu yeyote kama huyu anavyonena.
47Basi Mafarisayo wakawajibu, Je! Ninyi nanyi mmedanganyika?
48Yn 12:42 Ni nani katika wakuu amwaminiye, au katika Mafarisayo?
49Lakini makutano hawa wasioifahamu torati wamelaaniwa.
50Yn 3:1-2 Akawaambia Nikodemo, (naye ni yule aliyemwendea zamani, maana ni mmoja wao),
51Kum 1:16,17; 19:15 Je! Torati yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikia kwanza, na kujua atendavyo?
52Yn 1:46; 7:41 Wakajibu, wakamwambia, Je! Wewe nawe umetoka Galilaya! Chunguza, na utaona kuwa Galilaya hakutatoka nabii.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.