2 Samweli 9 - Swahili Revised Union Version DC

Daudi amhurumia Mefiboshethi

1 1 Sam 20:15-17; 18:3; Mit 27:10 Kisha Daudi akasema, Je! Amesalia mtu mmoja katika nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema kwa ajili ya Yonathani?

22 Sam 16:1; 19:17 Palikuwa na mtumishi mmoja wa nyumba ya Sauli, jina lake Siba, basi wakamwita aende kwa Daudi; na mfalme akamwuliza, Wewe ndiwe Siba? Naye akasema Mimi, mtumishi wako ndiye.

32 Sam 4:4; Kum 10:15; 1 Sam 20:14; Mt 5:44,45; Lk 6:36; Tit 3:3,4 Mfalme akasema, Je! Hakuna hata sasa mtu yeyote wa nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema ya Mungu? Siba akamwambia mfalme, Yonathani anaye mwana hata sasa, aliye na kilema cha mguu.

42 Sam 17:27 Mfalme akamwambia, Yuko wapi? Siba akamwambia mfalme, Tazama, yumo katika nyumba ya Makiri, mwana wa Amieli, katika Lo-debari.

5Basi mfalme Daudi akatuma watu, na kumwondoa katika nyumba ya Makiri, mwana wa Amieli, katika Lo-debari.

6Basi Mefiboshethi, mwana wa Yonathani, mwana wa Sauli akaenda kwa Daudi, akaanguka kifudifudi, akasujudu. Daudi akasema, Mefiboshethi! Naye akaitika, Mimi hapa, mtumishi wako!

7Mwa 43:18,23; 50:21; 1 Sam 12:19-24; Yer 52:33 Daudi akamwambia, Usiogope, maana bila shaka nitakutendea mema; kwa ajili ya Yonathani, baba yako, nami nitakurudishia mashamba yote ya Sauli, babu yako; nawe utakula chakula mezani pangu daima.

81 Sam 24:14; 2 Sam 16:9 Akasujudu, akasema, Mimi mtumishi wako ni nini, hata ukamwangalia mbwa mfu kama mimi?

92 Sam 16:4; 19:29; Isa 32:8 Ndipo mfalme akamwita Siba, mtumishi wa Sauli, akamwambia, Mali yote yaliyokuwa ya Sauli na ya nyumba yake nimempa mjukuu wa bwana wako.

102 Sam 19:17 Nawe utamlimia nchi hiyo, wewe, na wanao, na watumishi wako; nawe utamletea mjukuu wa bwana wako matunda yake, apate chakula ale; lakini Mefiboshethi, mjukuu wa bwana wako, atakula chakula mezani pangu siku zote. Basi huyo Siba alikuwa na wana kumi na watano na watumishi ishirini.

112 Sam 16:1-4; 19:24-30; Mit 12:17 Ndipo Siba akamwambia mfalme, Mimi, mtumishi wako, nitatenda hayo yote kama bwana wangu, mfalme, alivyoniamuru. Na kuhusu Mefiboshethi, mfalme alisema, Atakula mezani pangu, kama mmojawapo wa wana wa mfalme.

121 Nya 8:34 Huyo Mefiboshethi alikuwa na mwana mdogo, jina lake akiitwa Mika. Na watu wote waliokaa nyumbani mwa Siba walikuwa watumishi wa Mefiboshethi.

132 Sam 19:33,36; 2 Fal 25:29; Yer 52:33,34 Basi Mefiboshethi akakaa Yerusalemu; maana alikuwa akila chakula siku zote mezani pa mfalme; naye alikuwa na kilema cha miguu yote miwili.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help