Ezekieli 11 - Swahili Revised Union Version DC

Hukumu kwa washauri waovu

1 1 Fal 8:12; Eze 3:12,14; 8:3,16; 10:19 Tena roho ikaniinua, ikanileta hadi katika lango la upande wa mashariki mwa nyumba ya BWANA, lililoelekea upande wa mashariki; na tazama, mahali pa kuingilia pa lango walikuwako watu ishirini na watano; na katikati yao nikamwona Yaazania, mwana wa Azuri, na Pelatia, mwana wa Benaya, nao ni wakuu wa watu.

2Akaniambia, Mwanadamu, hawa ndio watu wale watungao uovu, na kutoa mashauri mabaya ndani ya mji huu;

3Yer 1:13 wasemao, Wakati wa kujenga nyumba hauko karibu; mji huu ni sufuria na sisi ni nyama.

4Basi toa unabii juu yao, Ee mwanadamu, toa unabii.

51 Nya 28:9; Zab 7:9; Yer 16:17; Yn 2:24; Ebr 4:11 Roho ya BWANA ikaniangukia, naye akaniambia, Nena, BWANA asema hivi; Mmesema maneno hayo, Enyi nyumba ya Israeli; maana mimi nayajua yaingiayo katika mioyo yenu.

6Mmewaongeza watu wenu waliouawa ndani ya mji wenu, nanyi mmezijaza njia kuu zake waliouawa.

7Mik 3:3 Basi Bwana MUNGU asema hivi; Watu wenu waliouawa, ambao mmewalaza katikati yake, hao ndio nyama hiyo, na mji huu ndio sufuria; lakini ninyi mtatolewa nje kutoka katikati yake.

8Mit 10:24 Ninyi mmeuogopa upanga; nami nitauleta upanga juu yenu, asema Bwana MUNGU.

9Zab 106:30 Nami nitawatoa ninyi nje kutoka katikati yake, na kuwatia katika mikono ya wageni, nami nitafanya hukumu kati yenu.

10Yer 39:6; 2 Fal 14:25; Zab 9:16 Mtaanguka kwa upanga; nitawahukumu katika mpaka wa Israeli; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.

11Yer 39:6 Mji huu hautakuwa sufuria lenu, wala ninyi hamtakuwa nyama ndani yake; nitawahukumu katika mpaka wa Israeli;

12Kum 12:30; Eze 8:10 nanyi mtajua ya kuwa mimi ni BWANA; kwa maana hamuendi katika amri zangu, wala hamkuzishika hukumu zangu, bali mmetenda mambo kama hukumu za mataifa wanaowazunguka.

13Mdo 5:5; Eze 9:8 Ikawa, nilipotoa unabii, Pelatia, mwana wa Benaya, akafa. Ndipo nikaanguka kifudifudi, nikalia kwa sauti kuu, nikasema, Ee Bwana MUNGU, je! Utawakomesha kabisa mabaki ya Israeli?

Mungu atastawisha Israeli tena

14Neno la BWANA likanijia, kusema,

15Mwanadamu, ndugu zako, naam, ndugu zako, watu wa jamaa zako, na nyumba yote ya Israeli, wote pia, ndio hao ambao wenyeji wa Yerusalemu wamewaambia, Jitengeni mbali na BWANA, nchi hii tumepewa sisi, iwe milki yetu;

16Zab 31:20; Isa 8:14 basi nena, Bwana MUNGU asema hivi, Ikiwa mimi nimewahamisha, wakae katika mataifa, na ikiwa mimi nimewatawanya katika nchi kadha wa kadha, pamoja na hayo nitakuwa patakatifu kwao kwa muda mchache, katika nchi zile walizozifika.

17Yer 24:5 Basi nena, Bwana MUNGU asema hivi; Nitawakusanya ninyi toka kati ya makabila ya watu, na kuwakutanisha toka nchi zile mlizotawanyika, nami nitawapeni nchi ya Israeli.

18Eze 37:23 Nao watafika huko, nao wataondolea mbali vitu vyake vyote vichukizavyo, na machukizo yake yote.

19Kum 30:6; 2 Nya 30:12; Yer 24:7; 31:33; Sef 3:9; Zab 51:10; Zek 7:12; Eze 36:26-28 Nami nitawapa moyo mmoja, nami nitatia roho mpya ndani yao; nami nitauondoa moyo wa kijiwe katika miili yao, nami nitawapa moyo wa nyama;

20Yer 11:4; Ebr 8:10; Eze 14:11; 36:28 ili waende katika amri zangu, na kuyashika maagizo yangu, na kuyatenda; nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.

21Ebr 3:12 Bali wao ambao mioyo yao huenda kwa kuufuata moyo wa vitu vyao vichukizavyo, na machukizo yao, nitaileta njia yao iwajilie juu ya vichwa vyao, asema Bwana MUNGU.

22Eze 1:19; 43:2-5 Ndipo hao makerubi wakainua mabawa yao, nayo magurudumu yalikuwa karibu nao, nao utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao.

23Eze 8:4; 43:4; Zek 14:4 Utukufu wa BWANA ukapaa juu toka katikati ya mji, ukasimama juu ya mlima wa upande wa mashariki wa mji.

24Eze 8:3; 2 Kor 12:2 Na roho hiyo ikaniinua, ikanichukua katika maono, kwa nguvu za Roho ya Mungu, hadi Ukaldayo, kwa watu wale wa uhamisho. Basi maono niliyoyaona yakaniacha.

25Mdo 20:20 Ndipo nikawaambia watu wa uhamisho habari ya mambo yote aliyonionesha BWANA.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help